Ni vizuri wananchi tuchukue nafasi ya kuwamulika viongozi wasiowajibika, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri kutokana na tuhuma mbalimbali zinazowakabili za matumizi mabaya ya madaraka, rushwa na miradi mingi kujengwa chini ya kiwango kwenye maeneo yao.
Hii inatokana na Mabaraza ya Madiwani hayana uwezo tena wa kuwasimamia Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi kwani kilichotokea Longido ndio kilichopo kwenye karibu Halmashauri zote kwamba madiwani hawakushinda bali walisaidiwa na Ma DC na Ma DED hivyo wanashindwa kuwasimamia na kushindwa kukemea uzembe, rushwa na ubabaishaji kwa hofu ya kutosaidiwa tena kwenye uchaguzi ujao.
Halmashauri sasa hazina wasemaji madiwani wako kimya, wabunge wako kimya mambo yanaharibika kwa hofu kuwa hawatasaidiwa tena uchaguzi ujao.
Ushauri Mamlaka zinazohusika ziwaondoe Ma DC na Wakurugenzi wote na kuteua wapya wenye weledi wataoweza kushirikiana na madiwani kuleta maendeleo sio hawa wanaowatisha madiwani kwamba hawakushinda basi Serikali ndiyo iliwaweka madarakani.