Kama mdau sihitaji kukanusha ila kueleza hali halisi. Katika mashindano haya kila timu ilitakiwa kuleta vitu vitatu, Kitambulisho cha Kazi, Bima ya Afya na Salary Slip. Taarifa hizi zilijulikana baada ya timu kufika Tanga. Timu hii ya WM ilipokatiwa rufaa, baadhi ya vithibitisho vilikosekana kwa timu zote mbili (Netball na Soka) hususan Salary Slip. Na kwasababu hiyo kwa mujibu wa kanuni ikalazimu zifutiwe matokeo licha ya kushinda mechi zake zote. Lakini kama wachezaji wote wangekaguliwa, kuna uwezekano mkubwa labda wasiozidi 20 ndiyo wangekuwa wana vithibitisho vyote vitatu.