Man Utd yafikia makubaliano na Sir Jim Ratcliffe, ambapo atamiliki 25% ya hisa za Klabu hiyo

Teko Modise

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2017
Posts
2,331
Reaction score
7,733
Hatimae kile kitendawili cha umiliki wa Man Utd kimeteguliwa leo kwa ambapo klabu hiyo imefikia makubaliano na Sir Jim Ratcliffe ambaye ni Mwenyekiti wa Kampuni ya INEOS kumiliki asilimia 25 Klabu hiyo.

Ikimbukwe wamiliki wa Man Utd bado watabakia familia ya Glazzer kwa asilimia 75.

Sir Jim ambaye ni mnazi wa timu hiyo atakuwa na jukumu la usimamiaji wa uendeshaji wa klabu hiyo kwa upande wa timu ya wanaume na wanawake.

Pia, Sir Jim atakuwa anashughulika na usajili wa timu, uboreshaji wa miundombinu na mambo mengineo ya klabu hiyo.

Sir Jim amemtangaza Jean-Claude Blanc kama CEO mpya wa Man Utd katika kuanza zama mpya za kuifufua timu hiyo yenye maskani yake kule katika kitongoji cha Cheshire, Old Trafford.
 
Sijawahi kuona ttz la glazers kwenye hii timu na hawawezi kuiachia timu kubwa kama hii kimasikhara tu
 
.itachukua zaidi ya Miaka 20 kwa manutd kutwaa kombe lolote kubwa post-Fergie era.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…