John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,374
Baadhi ya mshabiki wa soka wamemponda na kumdhihaki Cristiano Ronaldo mara baada ya kukosa penati na kushuhudi timu yake ya Manchester United ikiondolewa katika Kombe la FA dhidi ya Middlesbrough.
Ronaldo, 36, alikuwa na nafasi ya kuanza kufunga katika dakika za mwanzo kwa penati baada ya Paul Pogba kuchezewa faulo lakini alishindwa kufunga kwa kukosa mkwaju huo.
Matokeo ya bao 1-1 katika dakika za kawaidia yakasababisha timu hizo kupigiana mikwaju ya penati ambapo United ikaondolewa kwa 8-7.
Mashabiki mitandaoni walimrushia maneno ya kebehi Ronaldo kuwa amezeeka na hana uwezo tena, baadhi wakimuita Penaldo kwa kuwa tu hata uwezo wa kufunga penati hana.
Matokeo hayo yanaongeza presha kubwa kwa United hasa kwa kuwa wamekuwa na mwenendo mbovu tangu kuanza kwa msimu huu wa 2021/22.
Unadhani shida ni nini pale Manchester United? Ronaldo au kikosi kibovu au kocha hana uwezo?