Manara alijua mpira ni kauli mbiu

pwilo

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2015
Posts
10,913
Reaction score
13,876
Uhali gani shabiki wa soka nchini Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla? Poleni Yanga kwa kutoleawa kwenye CAF Champions League hapo jana, na hongera kwa wana Lunyasi kwa kuheshimisha taifa kwa mara nyingine tena. Ndio mpira huo, daima kuna nafasi nyingine, usikate tamaa.

Mpira wa Bongo una siasa nyingi sana na watu wamekuwa wakiziamini. Kama kuna mtu kawaingiza kingi Yanga Sports Club basi namba moja ni Manara. Kipindi Manara yupo Simba alikuwa anaaanzisha kauli mbiu katika kila mechi na hatua ya CAF Champions League na Simba ilikuwa inafanya vizuri na mashabiki wanajaa uwanjani.

Kauli mbiu kama:
~ WIDA – War in Dar es Salam
~ Kwa Mkapa hatoki mtu
~ Machozi jasho na damu
~ Total War

Na Simba ilipokuwa inashinda Manara alijiona shujaa na aliamini Simba inafanya vizuri kwasababu yake, kutokana na kauli mbiu zake. Kumbe siyo kweli, kauli mbiu peke yake haifanyi kazi mpaka uwe na wachezaji kweli kweli siyo wa kuungaunga.

Mungu si Athumani akaondoka kaenda zake Yanga, akilini mwake akajijengea Simba ilikuwa inashinda kwasababu ya kauli mbiu zake. Akaendelea na kauli mbiu kule Yanga, sasa kila kitu kimefeli.

Akaenda Yanga akaanza na; "The return of the Champions" ikafa kifo cha mende, akarudi tena na" Iwe Jua iwe Mvua". Kweli Manara ana "Ego" sana, anaamini bila yeye hakuna timu itafanikiwa bila yeye kuhusika. Ndio maana hata siku alipohojiwa, alisema yeye ndo alitoa wazo Yanga kupewa kombe mbali na Dar.

Kiufupi yule jamaa anapenda sifa, hata kufanya vibaya kwa Yanga na kufungwa na Al Hilal, anaamini ni kwasababu yeye amefungiwa. Angekuwa hajafungiwa Yanga ingefuzu! Kweli ule ni msekule unaoharibu brand na taswira ya Yanga pamoja na kugombanisha mashabiki na TFF.

Yanga tengenezi propaganda ya timu na kauli mbiu hazisaidii. Sawa Simba ni mbovu kama mnavyodai, ila Yanga kile ni kikundi cha wastaafu, kwa kule Ulaya ni kama Juventus inayochukua wachezaji waliocheza mda mrefu na wakakosa namba katika timu zao.

Yanga walijua kuingia makundi ni kitu rahisi, wakajifungia Kigamboni wakipata upepo safi wakisahau kule CAF Champions League hakuna bahasha za kaki na wachambuzi makanjanja, kila kitu kimenyooka. Sasa matumaini yamebaki Shirikisho huko, ambapo TP Mazembe na De Agosto wanawasubiria huko. Kila la kheri, ila maneno ya Manara yasiwaingize kingi tena. Mjipange muache janja janja.


NB: IWE JUA IWE MVUA MAKUNDI HAMUINGII, LABDA YA WHATSAPP.
 
Utopolo wametia aibu.

Simba anapambana kupeleka timu nne utopolo wanakuwa wa kwanza kuaga mashindano.

Iwe jua iwe mvua...sijui wanaenda kulima wapi?????
Rubish
Wanasema wanaenda kuchukua Caf confederation cup
 
Ni kweli na huwa anajiona shujaa kuliko kocha na wachezaji. Kumbe mpira unahitaji wachezaji wenye kujitoa na kuzingatia maelekezo ya mwalimu na si porojo za wasemaji.
 
mji umepoa umekua bardiiii[emoji23][emoji28]
 
Takadini anawaingiza mkenge Utopolo sana ikishinda Simba anakuwa na furaha isiyokuwa na kifani
Your browser is not able to display this video.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…