Manara anahangaika na hana washauri

Manara anahangaika na hana washauri

Albinoomweusi

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2016
Posts
3,433
Reaction score
8,585
Na adv. Mussa Makwinya

Nimepata bahati ya kumsikiliza mwamasishaji wa yanga Haji Manara kwenye press ya leo. Nimesikitika sana kwa baadhi ya maeneo ambayo ameyazungumza kwa hisia na kudhani anaonewa bila ya yeye au washauri wake kumpa ukweli wa mambo. Naomba niweke baadhi ya mambo ambayo naamini hajui atendalo au asemalo.

1) PINGAMIZI NA KESI YA MSINGI KUSIKILIZWA PAMOJA
Katika press yake amesema alishangaa kuambiwa kuwa pingamizi na kesi ya msingi vitasikilizwa pamoja na kusema haiwezekani jambo hilo na hata kwenye mahakama hakuna utaratibu huo. Nilishtuka na kujiuliza kama kweli alikuwa na wanasheria wabobezi kwenye eneo hilo. Na kama anao basi hakufuata ushauri wao. Kimsingi kilichofanywa na Kamati si kigeni kwenye tasnia ya sheria. Upo uwezekano wa kusikiliza pingamizi na kesi ya msingi kwa wakati mmoja na inafanyika mara nyingi mahakamani. Inapotokea hali hiyo, mahakama huanza kutoa uamuzi wa pingamizi (Ruling) na Kisha kama pingamizi halikuwa na mashiko ndipo uamuzi wa kesi ya msingi husomwa (decision). Aidha, endapo pingamizi linakuwa na mashiko hapo ndipo huwa mwisho wa kesi husika. Manara amelishwa matango pori kwenye eneo hilo au amejifanya kujua wakati hajui. Kwa mantiki hiyo, Kamati haikukosea kwenye hoja hiyo ya Manara.

2) KANUNI HAZIJASAJILIWA
Nilitegemea Manara angeueleza umma wa wanamichezo kuwa Kifungu au ibara fulani ya Katiba au Sheria ya BMT inaelekeza kuwa kila kanuni inayotungwa na klabu au Chama cha soka ni sharti kanuni hizo zisajiliwe ili hoja yake iwe na mashiko. Kinyume chake ameleta porojo, ili wanamichezo wasiopenda kusoma na kufanya utafiti waunge mkono porojo hizo. Ibara ya 63(3) ya Katiba ya TFF kinatoa mamlaka kwa Kamati ya utendaji kutunga kanuni zinazoendesha mpira kwa kuzingatia kanuni za FIFA. AIDHA, Sheria ya BMT inazitaka klabu kusajili Katiba zao na hakuna mahali inazitaka klabu kusajili kanuni zao za uendeshaji za kila siku. Kama sheria hiyo ingeweka takwa hilo TFF wangelazmika kufanya hivyo na hoja ya manara ingebeba mashiko. Kinyume chake hakuna kifungu wala kanuni zilizotungwa na sheria hiyo kinchoelekeza suala hilo. Kwa mantiki hiyo na kwa kuwa mpira huendeshwa na TFF kama taasisi huru, hujiwekea kanuni zake na namna ya kuzihalalisha. Madamu yanga na simba ni wanachama, kanuni zao zinapitishwa na Kamati tendaji kwa mujibu wa Katiba ya TFF ambayo klabu hizi ni wanachama. Hakuna asasi binafsi, hata zile zinazosajiliwa Wizara ya mambo ya ndani ambayo husajili kanuni za uendeshaji hadi pale sheria mahsusi inapoelekeza hivyo. Kinachosajiliwa kwa sasa ni katiba zao. Cha msingi kanuni zinazotengenezwa hazipaswi kukinzana na katiba zao na sheria za nchi. Hapa napo Manara ameongea porojo ili apate huruma za watanzania waache kujadili hoja ya msingi ya utovu wake wa nidhamu wake bali tujadili agenda anayoiingiza yeye na ambayo haipo.

3) NAKALA YA HUKUMU
Nikiri kuwa ni haki yake kama mfungwa wa mpira( au moja ya pande ya kesi husika), kupata nakala si ya hukumu tu bali mwenendo ( proceedings) wa shauri lake ili aweze kuifanyia kazi au kujua namna uamuzi wa hoja aliyofungiwa kwayo ulivyofikiwa na kama yale yaliyojadiliwa wakati wa kesi ndiyo yamehusika tu na si jambo lingine. Amedai ameandika kuomba nakala ya hukumu, hata hivyo suala la kupata nakala haulisubiri nyumbani hata kama kwenye mahakama za kawaida. Ni sharti ufuate nakala hiyo na mwenendo mahakamani. Haji hajatuambia lini alienda TFF akataka nakala akanyimwa. Bwana yule anavyopenda media kila mtu angeambiwa kuwa leo naenda. Kimsingi jukumu la kufuata nakala ni la kwake na wala si la TFf kuituma kwake. Ni kweli ameandika barua au kwenda TFF? kama ameweza kutoa nakala ya barua ya Hospitali ameshindwa nini kutuonesha nakala ya barua aliyoipeleka TFF kuomba hukumu? Mbaya zaidi waandishi wa nchi hii walivyotunyima haki hawakuhoji hilo na kupata ukweli. Hapa manara anataka tumwamini yeye na kuipa kasoro TFF wakati hajakidhi kiu ya maswali yetu ambayo waandishi wamekimbia kumuliza.

4) SERIKALI IUNDE TUME
Nimesikitika kusikia hoja hii kutoka kwa kiongozi kama yeye. Na kama hizi ndizo hoja za viongozi wa vilabu hivi, hasa yanga anayoitumikia basi tunayo safari ndefu kufikia mafanikio ya soka. Anajua vipo vyombo vya haki ambavyo anapaswa kuwasilisha hoja zake na bado hajafanya hivyo. Tume ya nini wakati bado vipo vyombo vya haki hajavifikia? Kwa mantiki ya hoja hii ndiyo maana hataki kwenda kuchukua nakala ya hukumu yake. Nimejiuliza, Tume ikachunguze nini? Matusi au hoja gani na kwa maslahi ya nani, je yeye ni mtu maalum kwenye tasnia ambaye akiguswa tu serikali iamke? Alikuwa na mawakili wake kwanini hawakuwasilisha hoja alizonazo wakati wa shauri? Nini maana ya kuwa na wakili?

Naomba kwa ajili ya muda niishie hapa kesho nitaendelea na hoja zingine
 
Naomba kwa ajili ya muda niishie hapa kesho notaendelea na hoja zingine
Umefafanua vizuri, mimi hoja yangu naona hizi kanuni za TFF zinatoa mwanya wa kutoa hukumu kwa kukomoana, kwa mfano kanuni inayosema faini isiyopungua milioni tatu bila kuweka ukomo, hii sio sawa.
 
Anazidi kuboa kila mtu atamchoka.
Hata Yanga wamemchoka ndiyo maana wakamjaza upepo aendelee kuropoka kama msemaji wao ilhali yuko kifungoni ili akipigwa kabari ya mbao na misumari akafie mbali na usimba wake uliojificha moyoni mwake. Amewafanya Yanga wapumbavu sana akiwa kwenye media anaongea hadi mishipa ya shingo inamsimama kuitetea Yanga lakini akiwa na watu wake wa karibu anasema yeye siyo chizi hadi awe Yanga pale anatengeneza maisha yake tu. Naona kuna watu wameshamstukia sasa wametumia staili kama ya Magufuli alivyomtosa Bashite kwa kumruhusu kwenda kugombea ubunge kigamboni akijua kuwa hatapita na ndiyo ukawa mwisho wake. Yanga kuna watu wana vichwa vinafanya kazi kicuba.
 
MANARA KIPINDI HIKI APIGE KIMYA TU KWANZA
Na angefanya hivyo angekuwa kwenye nafasi nzuri ya kujenga hoja zenye mashiko kwenye rufaa yake,lakini kwa hili alilofanya jana ndiyo amenyea kitanda anacholalia
 
😁😁😁
16588134714313.jpg
 
Na adv. Mussa Makwinya

Nimepata bahati ya kumsikiliza mwamasishaji wa yanga Haji Manara kwenye press ya leo. Nimesikitika sana kwa baadhi ya maeneo ambayo ameyazungumza kwa hisia na kudhani anaonewa bila ya yeye au washauri wake kumpa ukweli wa mambo. Naomba niweke baadhi ya mambo ambayo naamini hajui atendalo au asemalo.
1) PINGAMIZI NA KESI YA MSINGI KUSIKILIZWA PAMOJA
Katika press yake amesema alishangaa kuambiwa kuwa pingamizi na kesi ya msingi vitasikilizwa pamoja na kusema haiwezekani jambo hilo na hata kwenye mahakama hakuna utaratibu huo. Nilishtuka na kujiuliza kama kweli alikuwa na wanasheria wabobezi kwenye eneo hilo. Na kama anao basi hakufuata ushauri wao. Kimsingi kilichofanywa na Kamati si kigeni kwenye tasnia ya sheria. Upo uwezekano wa kusikiliza pingamizi na kesi ya msingi kwa wakati mmoja na inafanyika mara nyingi mahakamani. Inapotokea hali hiyo, mahakama huanza kutoa uamuzi wa pingamizi (Ruling) na Kisha kama pingamizi halikuwa na mashiko ndipo uamuzi wa kesi ya msingi husomwa (decision). Aidha, endapo pingamizi linakuwa na mashiko hapo ndipo huwa mwisho wa kesi husika. Manara amelishwa matango pori kwenye eneo hilo au amejifanya kujua wakati hajui. Kwa mantiki hiyo, Kamati haikukosea kwenye hoja hiyo ya Manara.
2) KANUNI HAZIJASAJILIWA
Nilitegemea Manara angeueleza umma wa wanamichezo kuwa Kifungu au ibara fulani ya Katiba au Sheria ya BMT inaelekeza kuwa kila kanuni inayotungwa na klabu au Chama cha soka ni sharti kanuni hizo zisajiliwe ili hoja yake iwe na mashiko. Kinyume chake ameleta porojo, ili wanamichezo wasiopenda kusoma na kufanya utafiti waunge mkono porojo hizo. Ibara ya 63(3) ya Katiba ya TFF kinatoa mamlaka kwa Kamati ya utendaji kutunga kanuni zinazoendesha mpira kwa kuzingatia kanuni za FIFA. AIDHA, Sheria ya BMT inazitaka klabu kusajili Katiba zao na hakuna mahali inazitaka klabu kusajili kanuni zao za uendeshaji za kila siku. Kama sheria hiyo ingeweka takwa hilo TFF wangelazmika kufanya hivyo na hoja ya manara ingebeba mashiko. Kinyume chake hakuna kifungu wala kanuni zilizotungwa na sheria hiyo kinchoelekeza suala hilo. Kwa mantiki hiyo na kwa kuwa mpira huendeshwa na TFF kama taasisi huru, hujiwekea kanuni zake na namna ya kuzihalalisha. Madamu yanga na simba ni wanachama, kanuni zao zinapitishwa na Kamati tendaji kwa mujibu wa Katiba ya TFF ambayo klabu hizi ni wanachama. Hakuna asasi binafsi, hata zile zinazosajiliwa Wizara ya mambo ya ndani ambayo husajili kanuni za uendeshaji hadi pale sheria mahsusi inapoelekeza hivyo. Kinachosajiliwa kwa sasa ni katiba zao. Cha msingi kanuni zinazotengenezwa hazipaswi kukinzana na katiba zao na sheria za nchi. Hapa napo Manara ameongea porojo ili apate huruma za watanzania waache kujadili hoja ya msingi ya utovu wake wa nidhamu wake bali tujadili agenda anayoiingiza yeye na ambayo haipo.

3) NAKALA YA HUKUMU
Nikiri kuwa ni haki yake kama mfungwa wa mpira( au moja ya pande ya kesi husika), kupata nakala si ya hukumu tu bali mwenendo ( proceedings) wa shauri lake ili aweze kuifanyia kazi au kujua namna uamuzi wa hoja aliyofungiwa kwayo ulivyofikiwa na kama yale yaliyojadiliwa wakati wa kesi ndiyo yamehusika tu na si jambo lingine. Amedai ameandika kuomba nakala ya hukumu, hata hivyo suala la kupata nakala haulisubiri nyumbani hata kama kwenye mahakama za kawaida. Ni sharti ufuate nakala hiyo na mwenendo mahakamani. Haji hajatuambia lini alienda TFF akataka nakala akanyimwa. Bwana yule anavyopenda media kila mtu angeambiwa kuwa leo naenda. Kimsingi jukumu la kufuata nakala ni la kwake na wala si la TFf kuituma kwake. Ni kweli ameandika barua au kwenda TFF? kama ameweza kutoa nakala ya barua ya Hospitali ameshindwa nini kutuonesha nakala ya barua aliyoipeleka TFF kuomba hukumu? Mbaya zaidi waandishi wa nchi hii walivyotunyima haki hawakuhoji hilo na kupata ukweli. Hapa manara anataka tumwamini yeye na kuipa kasoro TFF wakati hajakidhi kiu ya maswali yetu ambayo waandishi wamekimbia kumuliza.
4) SERIKALI IUNDE TUME
Nimesikitika kusikia hoja hii kutoka kwa kiongozi kama yeye. Na kama hizi ndizo hoja za viongozi wa vilabu hivi, hasa yanga anayoitumikia basi tunayo safari ndefu kufikia mafanikio ya soka. Anajua vipo vyombo vya haki ambavyo anapaswa kuwasilisha hoja zake na bado hajafanya hivyo. Tume ya nini wakati bado vipo vyombo vya haki hajavifikia? Kwa mantiki ya hoja hii ndiyo maana hataki kwenda kuchukua nakala ya hukumu yake. Nimejiuliza, Tume ikachunguze nini? Matusi au hoja gani na kwa maslahi ya nani, je yeye ni mtu maalum kwenye tasnia ambaye akiguswa tu serikali iamke? Alikuwa na mawakili wake kwanini hawakuwasilisha hoja alizonazo wakati wa shauri? Nini maana ya kuwa na wakili?
Naomba kwa ajili ya muda niishie hapa kesho notaendelea na hoja zingine
Unilateral judgment siyo uonevu
Kulingana na mazingira yatakayokuwepo- kama upande mmoja haukutoa ushirikiano maamuzi yanaweza kutolewa kwa kusikiliza upande mmoja

Nafasi ya rufaa inatoa fursa kwa kila upande kuwasilisha concern zake kuhusiana na hukumu tajwa kama zipo
Kuendelea na defensive arguments kwenye media na kutaka kuwafundisha mawairi kazi ni ulimbukeni wa hali ya juu
 
Nadhani kwa sasa mods muunganishe hizi threads zote zinazomuhusu Manara. Yani jamii forums huwezi ona kitu kingine, ni Manara tu.
 
Manara aliwahi kusema wenye akili pale Yanga ni babaake Sunday na raisi mstaafu. Sasa naanza kuona ukweli kuwa Manara aliona mbali sana. Yeye kafungiwa kwa kosa lake la kijinga kabisa lakini taasisi nzima ya Yanga imeingia kichwa kichwa kumtetea kuanzia viongozi mpaka wazee wa timu. Kibaya zaidi hamna anayemtetea kwa akili kwa kumpa ushauri akate rufaa mpaka ngazi ya mwisho ya maamuzi badala wanamdanganya afanye "press" ambayo anaropoka tu vitu havina maana. Na wazee nao eti wanataka kumuona raisi. Raisi huyu huyu aache kuwa "busy" na mambo ya msingi ya nchi hii kama reli ya umeme, bwawa la umeme, madawa hospitalini, n.k. halafu akabebe mzigo wa roporopo Manara kwa kweli hata watanzania watamshangaa raisi wao.
 
Back
Top Bottom