Manara: Ipo siku nitakuwa Rais wa nchi

Manara: Ipo siku nitakuwa Rais wa nchi

real G

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2013
Posts
5,227
Reaction score
5,299
DSC04441.JPG


Msemaji wa timu ya soka ya Simba Haji S. Manara, amesema kwamba anaamini kuwa siku moja ndoto yake ya kuwa Rais wa Tanzania itakuja timia, kwani ndio tamanio lake la siku nyingi.


Akizungumza kwenye kipindi cha [HASHTAG]#KIKAANGONI[/HASHTAG] kinachorushwa kupitia ukurasa wa facebook wa East Africa Television, Haji Manara amesema yeye kama mwanasiasa upande wa pili, ndoto yake kubwa ni kuja kuwa Rais wa nchi baada ya kuzichanga.


“Iko siku mungu akinipa majaliwa, nikazichanga karata zangu, nitakuja kuwa rais, ndiyo ndoto yangu, na ndio ndoto za wanasiasa wote duniani, unaona bunge lile!? kama kuna mwanasiasa ambaye hana ndoto ya kuwa Rais hawafiki watano, mwanasiasa yoyote ukishaingia, hizo ndio ndoto kuja kushika wadhifa wa juu, kama huna ndoto wewe hufai kuishi”, amesema Manara.


Kauli hiyo ya Manara sio mara ya kwanza kusikika akiitamka, huku akisistiza kwamba kwa kuwa yeye ni mwanasiasa mzuri na mkweli, pia ni kada wa CCM, anaamini atakuja kushika wadhifa huo mkubwa kwenye nchi.



Chanzo: EATV
 
Atakua albino wa kwanza kua raisi duniani.
Japo mie Manara si wa upande wangu,wala simfagilii ktk nafasi yake hapo Mikia fc, Ila siwezi n'a siungi mkono ulichocomment maana huu ni zaidi ya unyanyapaa mkuu.
 
Atakua albino wa kwanza kua raisi duniani.
Hii siyo nzuri Mkuu.

Ana haki ya kugombea kama Mtanzania mwingine yeyote.

Nina wasiwasi na CV yake kama itamruhusu kugombea uraias lakini siyo mambo mengine kama hayo uliyoyataja.

Binafsi siwezi kumpa kura yangu maana mikia fc yenyewe ameshindwa kuingoza, ataweza kuongoza nchi yenye mamilioni ya watu?

Level yake ni kuwa mwenyekiti wa kitongoji huko vijijini full stop.
 
Back
Top Bottom