Manara tuachie Simba yetu

funzadume

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2010
Posts
13,624
Reaction score
21,362
TUACHIE SIMBA YETU...............
1. Kijana Haji Manara, Maneno yangu sikia,
Kwanza zuia hasira, Pindi unapoomgea,
Haya mambo ya mpira, Wengi watakuchukia,
Tuachie Simba yetu, Na wewe kafanye yako.

2. Umezaliwa mjini, Ni nani wa kukataa,
Mambo yote ya kihuni, Haji wewe wayajua,
Simba tulikuamini, Leo waja kutunyea,
Tuachie Simba yetu, Na wewe kafanye yako.

3. Mgongano masilahi, Ndio umekuondoa,
Wenyewe tulikusihi, Hukataka kusikia,
Leo unatukebehi, Eti mechi twanunua,
Tuachie Simba yetu, Na wewe kafanye yako.

4. Kazi bila mkataba, Leo ndio watwambia,
Au sasa umeshiba, Sahani unainyea,
Eti malipo kibaba, Nani wamuongopea,
Tuachie Simba yetu, Na wewe kafanye yako.

5. Umekosa uweledi, Haya yangu zingatia,
Maisha na ukaidi, Utakuja kujutia,
Ongea kwa ushahidi, Si kama wakuonea,
Tuachie Simba yetu, Na wewe kafanye yako.

6. Tumefungwa na mtani, Sote tulinyong'onyea,
Sasa wewe kigamboni, Nini umekiendea,
Tumeona darubini, Mwanzoni ulikataa,
Tuachie Simba yetu, Na wewe kafanye yako.

7. Hautakiwi kubisha, Simba imekuinua,
Leo nyota unaosha, Inakujua dunia,
Wapenzi ulitukosha, Kidogo nakusifia,
Tuachie Simba yetu, Na wewe kafanye yako.

8. Wa mtukana tajiri, Kwamba anatuibia,
Huyo ndio mfadhili, Wengine wamekimbia,
Simba tuna mkubali, Tena twamfagilia,
Tuachie Simba yetu, Na wewe kafanye yako.

9. Na ubingwa mara nne, Mjini tunatanua,
Sasa ni nani mwingine, Atakae tuokoa,
Ana sajili mashine, Timu yetu inang'aa,
Tuachie Simba yetu, Na wewe kafanye yako.

10. Twashindana Afrika, Tumevuka Tanzania,
Biriana uhakika, Minyama tunajilia,
Japo tuta kukumbuka, Ila kwa sasa timua,
Tuachie Simba yetu, Na wewe kafanye yako.

11. Mishahara wachezaji, Ni nani anaetoa,
Hata nyinyi wasemaji, Nani mnamuendea,
Gharama uendeshaji, Wapi pa kukimbilia,
Tuachie Simba yetu, Na wewe kafanye yako.

12. Bodi ya wakurugenzi, Imekwisha kuamua,
Utabakia mpenzi, Timu kuishangilia,
Ila kwenye uongozi, Kamwaga amerejea,
Tuachie Simba yetu, Na wewe kafanye yako.

13. Ukitaka nenda Yanga, Ni timu ya familia,
Kwani achumae janga, Hula na wa kwao pia,
Figisu unazopanga, Puani zitatokea,
Tuachie Simba yetu, Na wewe kafanye yako.

14Simba ina songa mbele, Wenyewe tumetulia,
Itabakia milele, Sisi tuta tangulia,
Japo twapigwa mishale, Maumivu yatapoa,
Tuachie Simba yetu, Na wewe kafanye yako.

15. Shairi nalimaliza, Nimechoka kuongea,
Mengi nimeyaeleza, Wenyewe mmesikia,
Na kama nimeteleza, Samahani naitoa,
Simba timu kubwa sana, Zaidi ya sisi wote.
 
Haji aiche Simba,keshatoka atafute pakwenda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…