Pre GE2025 Manara: Utani wa Simba na Yanga umesaidia kuleta Utulivu nchini, utakuta Maji, Sukari na Umeme hakuna lakini Media zinajadili Simba na Yanga!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
 
tangu nianze kumsikiliza manara leo ndo kaongea jambo la kutafakari sana.........kwamba ushabiki wa simba na Yanga una manifaa kwa nchi yetu au ni hatari unaua vijana wengi.
Hata mimi najua ni chizi fulani hizi
 
Leo 99% busy walikuwa busy na story za Yanga huku majangili ya nchi yanakiiba vizuri
 
Labda huu ndio uchawi wenyewe
 
Leo 99% busy walikuwa busy na story za Yanga huku majangili ya nchi yanakiiba vizuri

Kinachonishangaza Mimi,hadi wasomi wa nchi hii ambao tulitegemea wangekuwa wakombozi wa hili taifa nao wamekuwa mazezeta ya kujadili Simba na yanga.

Leo nilishinda posta,Kila mahali unapopita ni mijadala juu ya yanga tu na swala la mahakama.

Wameshasahau hoja ya Nape.

Wameshasahau hoja ya yule jamaa wa chadema aliteteswa na polisi kule Tanga.

Inasikitisha sana. Simba na yanga ni zaidi ya dini hapa Bongo.
 
Wengine ni akina mwamposa ,upako nk,propaganda machines,
 
Ingawa ni kweli lakini fedheha tupu ila ongeza na uzinzi wa Diamond na Harmonize na porojo za Diva na Dida.
 
Hajaongea jambo jipya.Wengi tunaujua huo ukweli.
Siasa za Simba na Yanga sio za Kawaida.
Ule mgogoro wa kihisia baina ya Mtawala na Mtawaliwa kwa hapa Tanzania haupo kwa sababu ya Simba na Yanga.
Uhasimu huu umejipandikiza kwenye Michezo,na umekita mizizi.
Ule upinzani wa Yanga(timu ya wazawa) na Sunderland baadae Simba timu iliyokuwa imejaa wageni machotara wa kiarabu na wahindi nadhani Raia wengi wa wakati huo waliupenda na kuufurahia.
Kwani ulikuwa wakati Pekee wa wao kuwaonyesha wageni waliokuwa Raia wa Daraja la juu wakati huo kuwa wanaweza kuwazidi na kuwa Bora zaidi Yao.
Hata baada ya Uhuru timu hizi ziliendelea kuwa mahasimu mpaka leo.
Mapenzi ya Dhati kwa timu hizi watu wanarithishana vizazi kwa vizazi,mara nyingi huanzia majumbani mwetu.
Yanga ikichukua Ubingwa mpaka Jogoo mkubwa anachinjwa.
Mtu mzima Timu ikifungwa analia!.

As Long as Simba na Yanga wapo,Watawala bado wapo sana madarakani kwa Vizazi vingi vijavyo.Wanajua kilele Cha Furaha yenu kihisia Iko wapi.

Mfumo unatumia hii advantage vizuri sana.
 
Hao wasomi ,wauza magazeti,madalali, shoe shine,wauza kahawa,madereva taxi na wao hao ..baadhi wanakua kazini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…