Manara: Uwanja umeota mbawa, haya rudini bondeni mkahangaike na magugu maji

Manara: Uwanja umeota mbawa, haya rudini bondeni mkahangaike na magugu maji

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
8f912aa7de87e35af9ea3fef424a4857.jpg
Kufuatia Rais John Magufuli kuvunja Wakala wa Uendelezaji Mji wa Kigamboni (KDA) na kuelekeza shughuli zote za KDA zifanywe na Manispaa ya Kigamboni. Na kufuta umiliki wa mashamba mawili makubwa na kuyarudisha Serikalini likiwemo la Amadol lenye ekari 5,400 na lililokuwa likimilikiwa mfanyabiashara Yusuf Manji lenye ekari 715, ekari ambazo alizikabidhi Klabu ya Yanga African, maeneo ya Kigamboni Geza Ulole jijini Dar es salaam.

Hali hiyo imeyeyusha kabisa ndoto za Klabu hiyo kwa wakati huu wa miaka ya hivi karibuni kuwa na uwanja wa kisasa ambao ulikusudiwa kujengwa katika eneo hilo.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara ameandika kwenye ukurasa wake wa Instagram kuwa;

"Sijawahi kumdhihaki yeyote aliye katika mitihani coz siijui kesho yangu. Ila sitaacha kusema, Uwanja mliotutambia umeota mbawa, haya rudini bondeni mkahangaike na magugu maji", aliandika Manara.

Klabu ya Yanga ilikabidhiwa eneo hilo katika hafla iliyohudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba pamoja na Mke wa Rais wa kwanza wa Zanzibar hayati Sheikh Abeid Amani Karume, Mama Fatma Karume ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la wadhamini wa klabu hiyo ndiye aliyepokea eneo hilo.
ba9794eb99742ecf00ca4122165fff68.jpg
4d5ce192a5622ecc13a7ca6c1820fa9b.jpg
 
Haji Manara namuasa awe na akiba ya maneno
Manara mswahili hanaga hizo ila Yanga nao walibweteka na mali za Manji klabu ina miaka 80s bado tegemezi kwa kweli ni maajabu mengine ya dunia.
 
Manara mswahili hanaga hizo ila Yanga nao walibweteka na mali za Manji klabu ina miaka 80s bado tegemezi kwa kweli ni maajabu mengine ya dunia.
Kwani nyie simba vipi

Sent From My iDevice using Jamii Forums Auto-reply Mobile App
 
Manara mswahili hanaga hizo ila Yanga nao walibweteka na mali za Manji klabu ina miaka 80s bado tegemezi kwa kweli ni maajabu mengine ya dunia.
Exactly Mkuu. Ndo shida ya tegemezi , matokeo yake ni kumiliki dimbwi pale jangwani ambalo huwezi kufanyia lolote lile
 
Manara anahangaika na Yanga kama kama hawara anavyojipa majukumu ya mke halali [emoji23][emoji23][emoji23] timu ambayo inatusindikiza misimu 3 mfululizo badala wakae wafikirie ubingwa wao wako na Yanga kwa tabia hizi sintoshangaa ubingwa ukitetewa na Yanga tena kwa mara ya 4.
 
Hakuna wasiwasi wa ubingwa pale Msimbazi safari hii. Ikiwa mwaka jana chupuchupu pamoja na kubebwa kote na TFF
 
Manara mswahili hanaga hizo ila Yanga nao walibweteka na mali za Manji klabu ina miaka 80s bado tegemezi kwa kweli ni maajabu mengine ya dunia.
Ni kweli yanga na simba wote walikua tegemezi ila kwa sasa yanga inaonesha nia njema toka kwenye huo utegemezi na yanga wakiamua hili eneo wanarudishiwa bila wasiwasi bakini na hisa zenu zenye masharti kununua . Biashara haichagui mnunuzi unaposema atakae nunua hisa lazima awe mwanachama wa simba hunazuia raia wa kigeni kununua hisa as klabu pia unashusha thamani ya timu maana mwenye mtaji mkubwa kutoka nje ananyimwa fursa vilevile wajanja wachache unawapa fursa ya kumiliki timu kwa kufanya vikao vya na kununu japo asilimia 20 ya hisa kila mmoja na wao kua ndio wamiliki wakuu wa timu aka majority shareholder
 
Manara anahangaika na Yanga kama kama hawara anavyojipa majukumu ya mke halali [emoji23][emoji23][emoji23] timu ambayo inatusindikiza misimu 3 mfululizo badala wakae wafikirie ubingwa wao wako na Yanga kwa tabia hizi sintoshangaa ubingwa ukitetewa na Yanga tena kwa mara ya 4.
Manara anamtaka Salum Mkemi amemkosa ndo anaanza kusumbua.
 
Miundo mbinu mibovu lkn kwa wenzetu vyura ndio washazoea kuogelea madimbwini, wachache mtanielewa
 
Back
Top Bottom