Manara: Wanasema kikosi cha Simba kina thamani ya bil.1 umewahi kujua kama Chirwa pekee ana thamani ya mil.200?

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2012
Posts
2,046
Reaction score
3,971
Msemaji wa Simba SC Bwana Haji Manara anaongea na waandishi wa habari.

Katika maisha yangu sijawahi kuona mechi ya Yanga na Simba yenye mashabiki wachache kama ya juzi. Kumekuwa na ishu ya kuidhurumu Simba haki bila sababu kupitia waamuzi wetu haswa katika mchezo wa juzi

Yanga tumewapiga mechi nyingi wakiwa kamili Ngoma, Tambwe na wengine wote walionunuliwa fedha nyingi msimu uliopita. Wanasema kikosi cha Simba kina thamani ya bil.1 umewahi kujua kama Chirwa pekee ana thmani ya mil.200? Simba tulinyimwa Penalti mbili dhidi ya Mbao FC John Bocco aliangushwa lakini mwamuzi akakataa

Tunatumia gharama kubwa kuendesha hivi vilabu lakini mwamuzi anatoka nyumbani na matokeo. Tumewaandikia barua TFF na Waziri mwenye dhamana ya michezo kulalamikia haya maamuzi ya ajabu kwenye mpira. Benchi la ufundi Simba halina mabadiliko tunaendelea na kocha Omog na Juma Masoud na timu inafanya mazoezi
 
Kuna Watu Najua Watatoa Mapovu Hapa Kwa Kumuonea Wivu Manara Utazani Wao [HASHTAG]#YeboYebo[/HASHTAG] Hawana Msemaji Wao..
 
Na Wale Wambeya Waliopakaza Kuwa Omog Kafungishwa Virago, Manara Anasema Leo Jioni Waje Kwenye Mazoezi Ya Simba Watamkuta Omog Anaendelea na Mazoezi Kama Kawa..
 
Pia Kwa Wale Waliopakaza Simba Wamekata Rufaa! Manara Amekanusha Na Kusema Walichofanya Simba Ni Kupeleka Malalamiko Dhidi Ya Maamuzi Mabovu Ya Referees ili TFF ilione hilo na Kuweza Kuongea Nao ili Wajue Majukumu Yao na Si Kutoka Na Matokeo Majumbani Kwao..

MANARA: Maamuzi Ya Referee Uwanjani Akishayatoa
Hayapingwi. Kwahiyo Hatukukuta Rufaa bali Tumepeleka Malalamiko tu dhidi ya Ubovu wa Referee na Wala si dhidi ya Matokeo ya Mchezo..

Simba Hatudai Point yoyote Kwa Mechi Na Yanga lakini Tunataka TFF ijue Kuwa Waamuzi wake ni Mabashite.
 
hivi huyo mropokaji wenu anazo zote kweli? ipo siku atatembea bila nguo. mnaona anapoelekea halaf mnamwacha tu! kwahiyo kila mchezaji anapoanguka bac wapewe penati? dah! safari hii lazima muende ICC
 
Manara acha kulalamika, mpira ni uwanjani.
 
Yaani Simba kila siku kulalamika wanaonewa loh. Manara mpira upo uwanjani acha lawama
 
Manara anawajua vizuri mashabiki wa mikia baada ya mbwembwe zake kabla ya game anajua watakua wamemaindi sasa kuwapoza ndio anaibuka kama ivi huwezi amini mashabiki wa mikia watatulia na kuamini kua wanaonewa,ishu ya Omog iko wazi ni suala la muda tu hata mikia wanajua kua atakimbizwa.
 
Anajuta gharama kubwa ya usajili haileti tofauti na gharama ndogo ya usajili kwenye msimamo wa ligi, msimu ujao lazima wataachana na usajili wa gharama kubwa maana ni aibu kwa club yao.
 
Simba Hatudai Point yoyote Kwa Mechi Na Yanga lakini Tunataka TFF ijue Kuwa Waamuzi wake ni Mabashite.

Hivi Manara anajua kuwa ukitaja "Bashite" inakuwa umemlenga mkuu wake wa mkoa?!, au wanajuana kwa vile wote ni watoto wa mjini?
 
Km mkiwa na kiongozi ama awe mwanamke au ni kilema lazima kila Mara hiyo sehem itakuwa na malalamiko sababu hao watu wanakuwa wanajihisi hawako sawa na wengine kwahiyo kila wafanyalo watakuwa wanahitaji kuonewa huruma. Mfano spika Makinda alikuwa analalamika sana anaonewa sababu yeye mwanamke.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…