Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Inadaiwa Klabu ya Manchester City imeongeza jitihada za kutaka kumsajili nyota wa Klabu ya Arsenal na timu ya Taifa ya England, Bukayo Saka
Mabingwa hao wa England wanafuatilia kwa karibu mustakabali wa Saka katika Klabu ya Arsenal ambapo amebakiza miaka miwili katika mkataba wake
Hata hivyo, moja ya vipaumbele vya Arsenal majira haya ya joto ni kumpa Saka mkataba mpya ulioboreshwa utakaoendana na kiwango chake bora cha sasa