Manchester City imefanikiwa kutetea taji la Premier League msimu wa 2021/2022 baada ya kushinda mchezo wa mwisho wa ligi hiyo kwa mabao 3-2 dhidi ya Aston Villa, leo Mei 22, 2022.
Man City imetwaa umetwaa ubingwa huo kwa kufikisha pointi 93 huku Liverpool ikishika nafasi ya pili kwa kuwa na pointi 92 baada ya kushinda mchezo wa mwisho dhidi ya Wolves kwa mabao 3-1.
Licha ya kuwa nyuma kwa mabao 2-0 hadi dakika ya 75 katika mchezo wa leo, Man City ilirejesha makali na kupata mabao yake dakika ya 76, 78 na 81. Huo ni ubingwa wa 8 wa Premier League kwa Man City.