Mc cane
JF-Expert Member
- May 18, 2018
- 5,570
- 10,517
Baada ya miaka 17 ya umiliki wa Glazers family, iliyokumbwa na mikiki ya kukataliwa na mashabiki, sasa rasmi wameamua kuiweka klabu ya Man Utd Sokoni. Hili limetangazwa tarehe 22/11/2022.
Katika "statement" iliyotolewa na Bodi ya Man Utd na baadaye ikathibitishwa na Avram Glazer, wamiliki wa Man United wameamua kuweka milango wazi kwa wawekezaji wapya kuja kuwekeza (Glazers wakiendelea kuwa wamiliki) au kuiuza (kupata mmiliki mpya) au kuruhusu biashara katika klabu ili kuongeza pato la uwekezaji. Hata hivyo, inatajwa chaguo la kuinunua/kuiuza ndio chaguo lenye nguvu zaidi.
Kwanini Glazers wameamua kuiuza Manchester United?
1. Muendelezo wa mashabiki wa Man Utd kuwakataa Glazers kuwa wamiliki kwa miaka yote 17 ya umiliki wao.
2. Glazers kukosa fedha za kuirudisha klabu kuwa klabu tishio kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.
3. Glazers kukosa fedha za kuisasisha miundombinu ya uwanja wa Old Trafford na Carrington kuwa ya kisasa kama vilabu vingine vinavyofanya (Man City, Real Madrid wameboresha sana miundombinu yao hivi karibuni).
4. Mgogoro wa kiuchumi Duniani kumewanyima Glazers family fursa ya kupata mikopo yenye masharti nafuu kwa ajili ya kuwekeza Manchester United.
5. Anguko la Super League ambapo limesababisha uhusiano wa Glazers family na mashabiki kuzorota zaidi na pia umeinyima familia hiyo fursa ya mapato makubwa kutoka Super League.
Man Utd inauzwa bei gani?
Inatajwa kuwa Glazers wapo tayari kukabidhi timu kwa mtu/kampuni ambayo ipo tayari kulipa kiasi cha kati ya paundi bilioni 5 - 9. Hii itaifanya Man Utd kuwa klabu ya michezo ghali zaidi duniani, klabu inayoshika rekodi ni Denver Broncos klabu ya American Football (sio soka) iliyouzwa kwa paundi bilioni 3.9. Tusisahau Chelsea imeuzwa hivi karibuni kwa poundi bilioni 2.5 na Liverpool ipo sokoni kwa gharama ya paundi bilioni 2.7.
Je, mahojiano ya Ronaldo ndio yamesababisha Glazers kuamua kuiuza Man UTD?
Hapana, maamuzi ya familia kuhusu kuiuza Yanga yamefanyika kabla ya mahojiano ya Piers Morgan na Cr7. Taarifa ya kuiuza Man Utd ilitoka masaa 4 baada ya Cr7 kufanya mahojiano yale. Haiwezekani ndani ya masaa 4, familia ikae, kisha bodi ikae halafu watangaze maamuzi ya kuiuza klabu.
Lini Man utakuwa imeshauzwa?
Haiwezi kuwa kabla ya Januari na kama kila kitu kitakuwa sawa bila complications zozote, zoezi hilo litakamilika kabla msimu huu kuisha (May/June 2023). Kutazama time frame ya ununuzi wa Chelsea inaweza kukupa picha ya lini Man UTD itakuwa imeshauzwa.
Nani Wanaotajwa kuwa Wanaimendea Man UTD?
Matajiri wengi wanatajwa, kati yao ni:
1. Sir Jim Ratcliffe, mfanyabiashara tajiri zaidi Uingereza ambaye pia ni shabiki wa Man Utd. Thamani ya utajiri wake inatajwa kuwa ni paundi bilioni 10.9.
2. Matajiri wa mafuta kutoka Saudi Arabia na Dubai.
3. Wawekezaji kutoka Wamarekani.
4. Amancio Ortega tajiri namba 19 duniani, tajiri wa Kampuni ya Zara Fashion mwenye utajiri wa thamani ya dola za kimarekani bilioni 61.3.
5. Apple kampuni kubwa zaidi ya kiteknolojia yenye thamani ya paundi bilioni 2000.
6. Wengine.
Je, Glazers wanaiuza klabu kwa hasara?
La hasha, miaka 17 Glazer Snr alinunua Manchester United kwa paundi milioni 790, milioni 600 kati ya hizo walikopa na baada ya kuinunua mkopo ukahamishiwa kwenye klabu ya Manchester United. Endapo wataiuza klabu kwa paundi bilioni 5, watakuwa wametengeneza faida ya zaidi ya asilimia 600, tena kwa hela ya mkopo ambao kwa sasa ni klabu ndiyo inadaiwa.
Mashabiki United wanasemaje?
Mashabiki walio wengi wanatamani klabu ya Manchester United ibadili mmiliki ambaye ataimarisha miundombinu ya klabu na kusajili wachezaji watakaoirudisha klabu katika enzi za ufalme wake.
Bila kujali ni Wamarekani, Wasaudia, Wadubai, Wachina, Wahindi au Waingereza... Mashabiki wengi wanataka mmiliki mpya mwenye pochi nene ya kuiletea mapinduzi makubwa klabu ya Manchester United.
Sent from my M2004J19C using JamiiForums mobile app