Manchester United ni Marketing genius

marcoveratti

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2017
Posts
1,019
Reaction score
1,824
Kabla sijaenda kwenye jezi na marketing strategy ya mauzo ya jezi kati ya Manchester united na Adidas nakurudisha nyuma kidogo miaka ya juzi juzi kwenye tamasha kubwa Zaidi Tanzania la FIESTA, wakati liko chuni ya Marketing Genius Ruge Mutahaba( RIP role model)

Mwaka ule FIESTA walikua wana tambulisha mfumo wa 100% local mfumo ambao haukuwahi kutimika kabla.

Na ikumbukwe kimsingi zaidi ya 70% ya wanaoenda Fiesta walikua wanaenda kufata wasanii wa kigeni ambao huwa wanaowaonaga tu kwa kideo,kama kina Rick Ross na wengine ambao wameshawahi kuja kupiga kazi zao nchini.

Swali la kwanza ni kwamba unawatoaje nyumbani hawa raia ambao ni zaidi ya 70% wanao fata wasanii wa kigeni waje fiesta yenye wakina nandi pekee?

Hapo ndio anapokuja marketing Genius na kutia mifumo yake sumu, na kuwatoa mapangoni hawa 70% ya Mashabiki wa fiesta ambao wanacho kufata hakipo.

Kwanza kabisa kibishara mnunuzi au mtumia huduma anakua na njia mbili ya kwanza kununua bidhaa na yapili kuto ninua bidhaa ,!
Hasa pale unapo badiri maudhui au kupunguza ubora wa bidhaa au hata kuongeza ubora basi mnunuzi wako anakua kwenye upande wa kutonunua hasa ukiachilia mbali wale loyal customers ambao kwa namna yoyote wao watanunua na kutumia huduma yako.
Customers ambao wanao Apple pekeao!

Kutokana na bsababu hii inatakiwa kumtoa mteja kwenye machaguo mawili ya kununua ama kuto nunua na kubaki na moja tu la kununua ...HOW !

FIEST walikuja na mpango mkakati wa kusema tamasha mwisho saa sita yani kwamba serikari imepiga mrufuku mpaka asubuhi.

Hapa automatic watu wakahama kwenye kwenda na kutokwenda kwa sababu ya 100% local na kubaki na kwenda na kuto kwenda kwasababu ya tamasha kuishia saa 6.

Raia ote wakatolewa mchezoni hahah! Baada ya kuhakikisha otee wamesha hama Marketing Genius akatoa order "tangazeni kibari cha tamasha mpaka asubuhi kimepatikana"

Mitaa ikapiga sana nduru hivyo mashabiki wakabaki na option moja tuu ambayo ni kwenda mana tamasha ni mpaka asubuhi masuala ya local na wasanii wageni yakafia hapo!
tamasha likajaa na watu wakaenjoy.


Twende sasa kwenye hoja ya msingi !

Manchester united wametoa Third kit yao ya zebra decoration ambayo kila mtu anaponda kwa nguvu zake zote kua jezi ni mbaya kupindukia. Yes! Jezi ni mbaya tena ni mbaya mno! Swali ni kwamba wao haoni kama ni mbaya hadi waka itoa na kuipeleka sokoni ?
HAPANA!

Manchester united wana untaratibu wa pre release ,yani wanatoa jezy decoration kama imevuja hivi kabla ya official release ili waone je? Fans wana comment vipi kuhusu jezi zao mpya.

Baada ya hapo wanafanya mabadiriko kama kutakua na umuhimu huo au kama hakutakua na umuhimu wana release ..

Kimsingi walikua wanajua jezi ni mbaya na haita pendwa ,lakini wamepeleka sokoni hivyo hivyo ..

Kwanini!, ?

Msimu ulio pita Manchester united wanakadiriwa kupoteza zaidi ya paund 20 milioni kwenye mauzo ya jezi kutokana na watu wengi kununua jezi za tatu badara ya zile za kwanza kwakua walivutiwa zaidi na jezi za tatu ambazo pamoja na kua nzuri pia gharama sake zipo chini!

Ikumbukwe bei ya jezi za tatu ni tofauti kabisa na ile ya jezi ya kwanza na ya ugenini mana quality ni tofauti pia

Hii imetokana na nini ni kwa sababu mashaniki walikua na machaguo mawili na wakaangulia kwenye chaguo ambalo haliwamufaishi adidas na Manchester united kimapato,

hapo ndio wataalamu kwakaa na kuskuti wakaona wasipo toa jezi za tatu ni jambo ambalo haliwezekani hawata eleweka .

Wafanyenyeje ! Jibu ni kama lile la fiesta "kuwatoa mashabiki mchezoni". Wabaki na na chaguo moja tuu la jezi ya kwanza na la pili basi machaguo ambayo yanafaida zaidi kwa Manchester united hasa wakati huu wanao tegemea kumleta Jason Sancho.

Anatwa Ed Woodward ,mwisho wa msimu nitarudi na takwimu za timu zilizo piga mpunga mrefu kupitia mauzo ya jezi lakini namba moja ni Manchester united kuendelea huko kuanzia mbili tusubiri msimu uishe

Mpaka sasa Manchester united ndio iko juu kimauzo ya jezi za 2020-2021 na majezi yao mabaya!
 
Upuuzi mtu yaani uuuze jezi kwa kutoa jezi isiyopendwa na watu Man U kweli njaa kali.

Kwanini wasitoe jezi nzuri watu wanunue akili imefika mwisho kwenye ubinifu.

Jezi mbaya watu wanunue kushinda jezi nzuri,uongo wazi wazi.eti wamefanya makusudi.
 
Acha upuuzi mleta mada, umesahau aliyesema fiesta mwisho saa sita ni yule mwenye maumivu ya wajumbe kule kigambonino
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…