marcoveratti
JF-Expert Member
- Sep 21, 2017
- 1,019
- 1,824
Kipindi cha Sir Alex Ferguson yeye ndie alikuwa mfalme hakuna mchezaji aliyekuwa ana nguvu au kuonesha makucha mbele yake. Ndio maana kuna nyakati aliwaondoa wachezaji kama Jaap Stam, David Beckam na Roy Keane ili kuwakumbusha watu klabu ni kubwa na ina nguvu kuliko wachezaji.
Wachezaji ni watu wa kupita tu kwenye timu.
Falsafa hizi ndizo wanazitumia makocha wa mpira Kama Gadiola na Klopp ndio maana wamefanikiwa sana .Kuna nyakati Klopp alimuondoa Coutinho baada ya kuota mapembe ,kuna nyakati Gadiola alimuondoa Joe Hart na Yaya Toure baada ya kuona hawafiti kwenye mfumo wake .
Hii inaonesha jinsi gani vilabu vya Liverpool na Mancity walivyotambua thamani ya timu zao ni kubwa kuliko hawa wachezaji kwani ni wapitaji tu.
Kwa sasa Manchester United wachezaji ndio wana nguvu na kupewa kipaumbele kuliko hata makocha, ndio maana unaona kuna nyakati tofauti walimuondoa Van Gaal,
huyu kufukuzwa kwake ilitokana na timu kushindwa kufuzu michuano ya Uefa mwaka 2015 licha ya kubeba FA cup.Manchester United waliamua kumleta Jose Mourinho kocha ambaye aliweza kuwapa Carling cup ,Ngao ya hisani na Europa league.
ila walifanya nini?, waliamua Kumfukuza Jose Mourinho ili kumrizisha mchezaji mmoja tu Pogba .
Tangu Manchester United wafanye maamuzi haya wachezaji wamekuwa na nguvu sana na kujiona wakubwa kuliko kocha au timu.
Wanajiamulia tu muda gani wacheze vizuri na muda gani warukeruke uwanjani,bado wachezaji hawa wameendelea kupewa mikataba minono huku Manchester United ikiwa ndio timu inayoongoza kulipa mishahara mikubwa ligi kuu England licha ya kufanya vibaya uwanjani.
Wachezaji wamekuwa wakipiga pesa huku mafanikio uwanjani hayaonekani zaidi ya kumaliza ndani ya Top 4.
Ole Gunnar Solkjaer ndie kocha pekee aliyejitahidi kuwadekeza wachezaji hawa aliwabusu mikono yao na kuwapigia magoti watu kama Pogba ,Rashford ,Martial wasimuangushe uwanjani.
Walijitahidi kucheza vizuri kwa kiasi chao ila pale walipomchoka Solkjaer naye waliamua kumtoa sadaka kama Jose Mourinho.
Hawakuangalia unyenyekevu wao kwao .Ndivyo walivyo kwao Manchester United pesa ndio kila kitu kucheza mpira baadaye.
Sasa amekuja Profesa wa mpira "Ragnick "mwenye falsafa za genging pressing . Walijaribu kuficha makucha yao na sasa wameamua kuyaonesha.
Inasikitisha kuona mchezaji wa kawaida kama Like Shaw ambaye na uhakika hawezi kupata namba kwenye vikosi vya Liverpool ,Mancity ,Chelsea naye anakosoa mbinu za Ragnick .
Mbinu za Ragnick zipo sahihi tu na mfumo wake wa 4-2-2-2 ndio maana alifanikiwa Schakle 04 na Rb Leipzg .Shida ya hawa wachezaji wetu wengi ni wavivu hawana hadhi ya kuchezea timu kubwa kama Manchester United na hawako tayari kukimbia kiometa nyingi uwanjani.
Suhulisho pekee ni kuwaondoa wachezaji mizigo Manchester United ,hakuna faida tutakayopata kwa wachezaji hawa wengi ni mizigo .
Kwa bahati mbaya wanaua nguvu za wachezaji wachache wanaojitambua kama ,Cavani ,Greenwood ,Varane ,Degea ,Ronaldo ,Sancho ,Mctomminay ,Fred ,Dalot ,Telles hata Van Beek ,Bally ,Lindelof ,Elanga ,Amad ,Mehjibir,Bruno Fernandes na Jones .
Hawa ndio wachezaji wachache nawaona bado wana moyo wa kuipambania Manchester United.Rashford ana moyo ila yuko bize na mambo ya nje ya uwanja.
Ni maamuzi magumu tu ya kuwaondoa wachezaji wengi mizigo ndio yanaweza kuisaidia Manchester United .Bila hivyo hii timu itaendelea kubaki kwenye giza la muda mrefu lisilokuwa na mwanga maana tayari kila kitu kinajionesha wachezaji ndio wana matatizo pale hawajitambui na siyo makocha wanao angushiwa jumba bovu kila wakija kufundisha Manchester United .
Wahenga wanasema "unapotaka kuondoa tatizo anza kwanza kukata mizizi ".Manchester United wajitafakari na wachukue hatua sahihi kuikoa timu hii iliyotengezwa na Sir Alex Ferguson karibia miaka 25.
Heshima ya timu iliyotengenezwa kwa muda mrefu ishushwe na wahuni wachache.
Ni maamuzi magumu tu yanayoweza kuiokoa timu hii "Unapotaka kumuua Nyani usimuangalie usoni "Manchester United wajitafakari na wachukue hatua kwa maslahi ya timu nzima.