Peculiar
JF-Expert Member
- Apr 5, 2015
- 821
- 689
Kwanza nianze kumpongeza kwa anachokifanya,si kwamba nampongeza kwa kupigwa pigwa la,ila kwa kutumia fursa.waswahili wanasema "bahati haiji mara mbili" na "mungu akitaka kukupa hakuandikii barua"
Mandonga licha ya kupoteza kwa kupigwa kwa aibu katika mapambano yake.bado hajawahi kuonesha unyonge.hajawahi kuonesha kukata tamaa.niseme tu kwa kifupi "mandonga ANA UWEZO MKUBWA WA KUHIMILI AIBU NA DHARAU,Lau asingekua kua na uwezo huo basi angeshaacha ngumi kitambo kwa mtazamo wangu.wala asingependa hata kusikia akiongelewa maana hata yeye anajijua Hana anachofanya ulingoni,zaidi ya kujitia aibu.
Lakini kwa kuwa ameweza kuishinda hali hiyo basi kwa kuwa KIPAJI CHAKE NI KUONGEA na si masumbwi basi ANATUMIA MDOMO WAKE kuyabadilisha madhaifu yake ya ulingoni kuwa fursa nje ulingo.
HIKI NI KIPAJI KIKUBWA SANA,japo wengi wanaweza kuchukulia poa.
ACHA APIGE PESA
Ni wakati wake, namuombea tu asiwe kwenye mikono ya wahuni,akawa anaumia yeye halafu wanufaika wakubwa wakawa wengine.sitamani kuja kusikia mandonga akija kulalamika baadae kwamba 'ooh nilidhurumiwa' ooh Sina hela' na vitu kama hivyo.
Nasema hivi maana mandonga kajitoa sana,mandonga hapigani kwa ajili yake peke yake,wapo wengi nyuma yake ambao kama mwanaume anapambana kwa ajili yao. Na kwa jina lake,na ushawishi wake wa kwa wakati huu anastahili KULIPWA VIZURI.
MANDONGA NGUMI HAJUI!
Japo mimi siujui huu mchezo kiundani ila sioni tabu kusema mandonga sio bondia. Mwanzo nilikua nasema labda atabadilika kwenye mapambano yanayokuja,ila naona anazidi kuwa mzembe ulingoni
Hajilindi kabisa
Ngumi zake nyepesi
Miguu inalegea mapema sana
Hayuko makini na anachokifanya ulingoni, Yuko makini zaidi na kelele za nje ya ulingo.
NAHISI HATA (MWALIMU HANA).
NAMKUBALI SANA MANDONGA
Anatoa funzo kwamba riziki huja kwa njia yoyote,haupaswi kujisikia mnyonge na kujifichaficha unaposhindwa kwenye lolote. Kwa kuwa hamuibii mtu wala hamdhurumu mtu, acha apige maisha.
MWISHO NISEME
Bado Mandonga anahitajika sana, kuna matukio mengi yatamuhitaji kukusanya watu na kusherehesha.
Hivyo usalama wa afya ya akili na mwili wake ni muhimu vikalindwa kwa manufaa yake na ya anaowapambania nyuma yake.
Ushauri wangu, apumzike ngumi kwa muda, ila kwa kuwa ndio kazi yake basi kama atashiriki, ahusike kama MSHEREHESHAJI (MC) na si mpiganaji.
Ni mtazamo tu