Mwande na Mndewa
JF-Expert Member
- Feb 26, 2021
- 1,117
- 3,153
Leo 13:15hrs 04/09/2022
Mandonga, shujaa wa ulingoni mwenye ujuzi mkubwa na mbinu za kuvutia, tekniki na ubora wa hali ya juu, timamu wa akili ya ngumi, mwepesi wa mwili mwenye kipaji cha kuzaliwa cha masumbwi, si mpiganaji mjanja bali mpiganaji mwenye skills zilizokwenda mbele zaidi kwenye makabiliano.
Bondia mwenye kipaji cha kuzaliwa aliyeanza kupigana ngumi akiwa tumboni mwa mama yake, amesema anamtaka Mwakinyo ili ampige kama ngoma. Mandonga amepinga utetezi wa Mwakinyo wa changamoto ya kubana kwa viatu kwa madai ya kupoteza bei airport.
Mandonga anasema waluguru na wadigo ni watani lakini Mwakinyo kawaangusha wadigo na amemshauri aache uwoga akiwa anapiga Marekani. Hata akienda Texas kwa mabingwa Mike Tyson au Stone Cold Austin au Shawn Michael asiwe na uwoga, ateme cheche kwenye tv na aende akampige mpinzani wake kama ngoma.
Mashabiki wake kama RJ Promotion wanasema uzuri wa mtu kazi ishu ya viatu haiwezi mpa shida. Mandonga anasema boxing sio mieleka ile, alipopigiwa Mwakinyo ile inaitwa corner unapigwa vizuri tu. Ameuliza kwanini Mwakinyo akubali kusogezwa mpaka kwenye kamba? Halafu hakuwa chini, mpaka ukae au udondoke kabisa chini ndo inahesabika faulo, refa aje kukuokoa ila siyo kupiga goti kama alivyokuwa amefanya Mwakinyo.
Mandonga amemtaka Mwakinyo ambaye yupo nchini Marekani hivi sasa, aongeze bidii nae apigane wiki kwa wiki kama anavyofanya yeye Mandonga, ajenge stamina au aje Morogoro tuendeshe tairi ya trekta kupandisha vilima vya Uluguru. Hii itamsaidia akiwa bingwa asije kuvuliwa ubingwa kwa kupigwa.
Mwakinyo amewahi kuvuliwa ubingwa wa mabara wa WBF na pia Mwakinyo alivuliwa ubingwa wa Afrika (ABU) kwa hizo hizo za kukataa kupigana. Mandonga anasema Mwakinyo is not a "fighting champion".