SoC03 Maneno 999 ya Taifa lenye amani na uzalendo wa juu

SoC03 Maneno 999 ya Taifa lenye amani na uzalendo wa juu

Stories of Change - 2023 Competition
Joined
Dec 10, 2020
Posts
15
Reaction score
14
Mwongozaji
Ni muda umepita sasa tangu sherehe hii ianze, watu wanaendelea kushangilia na kupiga makofi ya nderemo kwa taifa lao. Watu wengi wametamba na kujivunia taifa na uhuru wao, mwongozaji anaingia jukwaani na kuwakaribsha watu wa taifa hili waanze kutoa ahadi ya uzalendo wao.

Mwananchi wa kawaida
Anaingia jukwaani watu wanamshangilia anachukua kipaza sauti na kuanza kusema, "ninajivunia taifa langu, nitafanya kazi zangu kwa bidii, ninaahidi kulilinda taifa langu kwa kuhakikisha amani inakuwepo, nitafanya kazi zangu katika taifa langu kazi hizi zinanipatia kipato, ninapofanya kazi kwa bidii najisikia vizuri sana, amani iliyopo inaninifanya kujisikia faraja ninajivunia taifa langu, sitaacha kazi na sitajihusisha na vitendo viovu kwa ajili ya taifa langu, nina uhuru wa kutosha, Asanteni sana!" Anashukuru na kushuka jukwaani, watu wanamshangilia kote.

Mkulima.
Anaingia jukwaani anafuraha, anasimama na kushika kipaza sauti anaita kwa sauti "ndugu zanguuuu" ukumbi unaitika kwa makofi vigeregere na vifijo. Anasema "taifa letu haliwezi kufa, nitalipigania nitasimama kama mkulima kuhakikisha ninazalisha chakula kwa ajili ya familia yangu. Ninaamini familia inapokuwa na chakula ninalisaidia taifa. Chakula kinatoka shambani na mimi ninajivunia kazi hiyo na taifa linajivunia, kazi yangu inajenga taifa, amani na utulivu uliopo idumu vizazi na vizazi bila kuisha ili tuendelee kuishi kwa furaha katika taifa letu. kazi zetu tufanye kwa amani. tunajivunia taifa letu" kelele zinaitika za kushangilia maneno haya na mkulima anashuka.

Mwalimu
Anaingia jukwaani, watu wanamshangilia wanaimba Ujuzi! Ujuzi! Ujuzi! Ujuzi! Ujuzi! Ujuzi! wanamshangilia wanaamini anawapa watoto ujuzi na maarifa kwa kazi yake, anashika kipaza sauti na kusema ninajivunia taifa langu, ukumbi unasikika kwa shangilio la makofi mengi yanayopigwa bila kusita. Anaendelea na makofi yanasita, "nitafanya kazi yangu kwa bidii, watoto wenu ni watoto wangu" watu wanashangilia na kumfanya asite kwa muda na baadae kidogo anaendelea, ninafanya kazi hii kwa ajili ya taifa langu, ninawapenda watoto nitawasimamia katika maadili na malezi mema nitawapa ujuzi na maarifa ya kutosha kwa nguvu zangu zote ili kuhakikisha ninazalisha taifa bora, ninajivunia hilo na kazi hii, anasisitiza, hata nikiondoka duniani nitaacha taifa nililolitengeneza kwa mikono yangu, naipenda nchi yangu" Watu wanashangilia kote na anashuka jukwaani huku akipokelewa na makofi mengi.

Daktari
Anaingia jukwaani na watu wanaimba Uhai! Uhai! Uhai! Uhai! Uhai! wanamshangilia wakimaanisha anahakikisha uhai kwa wagonjwa. Anashika kipaza sauti na kusema, nina furahaaaaaa! Watu wanashangilia kwa nguvu, anaendelea huku wakimsikiliza na uso wa kila mmoja unaonesha furaha, anasema " ninajivunia taifa langu, nitafanya kazi yangu kwa bidii nitampa uhai mtu kwa uzalendo, nitahakikisha taifa linakuwepo kwa kuponya wagonjwa ili wapate afya warejee kulitumikia taifa katika kazi zao, nitafanya kwa bidii zangu zote sitachoka kwa upendo mkubwa kwa taifa langu, kila mmoja nitampa huduma kwa haki sawa bila ubaguzi, nitampa kila mgonjwa afya si maskini si tajiri, si msomi, si mtoto, si mzee si yeyote atakayebaguliwa wala kutoa chochote kwa ajili ya huduma. Watu wanashangila zaidi na anashuka huku akiendelea kushangiliwa sana.

Mwanasayasansi
Anaingia na kushangiliwa kama kawaida, watu wanamshangilia sana anachukua kipaza sauti na kusema, nitafanya majaribio mbalimbali ya kutatua matatizo mbalimbali kwa ajili ya taifa langu, watu wanashangilia kwa makofi mengi, anaendelea, nitajitahidi kwa juhudi zangu zote kufahamu vyanzo vya matatizo yote na kuyapatia utatuzi wake sahihi. Sitaki kuona taifa lina matatizo tutajua viini vya maradhi na tutafahamu namna ya kuvidhibiti na mengine mengi. Kila mtu atanufaika na matunda ya kazi yangu, taifa langu litanufaika. Anapaza sauti "ninajivunia taifa langu!) Watu wanashangilia anashuka jukwaani.

Mwanateknolojia
Anaingia jukwaani na kupaza sauti " ninajivunia taifa langu!, Ninajivunia taifa langu! Kadiri anavyotaja ndivyo watu wanashangilia zaidi. Anaendelea kwa kusema, "nitatengeneza vifaa mbalimbali kwa ajili ya taifa langu, nitatatua matatizo mbalimbali ya vifaa vya kazi na kiteknolojia kwa ajili ya taifa langu sitachoka nitavumbua na kuvumbua akili yangu haitalala anapaza sauti, "nalipenda taifa languuuu!". Kwa amani hii iliyopo nitahakikisha inaendelea kudumu kwa kutumia taknolojia thabiti kutoka kichwani mwangu kwa ajili ya taifa langu. Nitahakikisha napata nyenzo kwa kutumia maarifa makubwa, nitakapohitaji msaada myanipa najua " nitafanikiwa", wote wanaitika na kumshangilia ndiyoo! ndiyoo! ndiyoo! "Ninalipenda taifa langu" anamalizia na kushuka huku akishangiliwa.

Mwanajeshi
Anaingia huku akishangiliwa Shujaa wa amani! Shujaa wa amani! Shujaa wa amani! anapiga saluti na kushika kipaza sauti anaongea "kazi yangu naipenda sana, taifa langu nalipenda nitaifanya mpaka kufa, amani haitatetereka, nalipenda taifal langu, anaongea kizalendo na kwa upendo mkubwa, "nitadhibiti machafuko" hana maneno mengi anapiga saluti na kushuka watu wanamshangilia.

Hakimu
Anapanda jukwaani watu wanashangilia anasema, haki iko katika dhamana nitatoa haki, jambo moja tu kwa taifa langu ni kutoa haki yenyewe. Anaahidi nitahakikisha natoa Haki! Haki! Haki! Naipenda nchi yangu. Anashangiliwa na anashuka.

Polisi
Anaingia na kupiga saluti, anapigiwa makofi, anashika kipaza sauti na kusema, sitaki kumwonea raia asiye na hatia nitafanya uchunguzi wa kina ili kutokumwonea raia nitafanya hivyo ili haki itendeke nitakaa mbali na rushwa nikienda kinyume sisitahili taifa hili. Naipenda nchi yangu. Anashuka na anashangiliwa.

Mwandishi wa habari
Anaingia ukumbini anashika maiki, anapaza sauti inayosikika kwenye spika, kazi yangu ni kutoa taarifa, nitakuwa makini kwa kila mtu kwa maana kama nitatoa taarifa isiyo halali ninalikosea taifa langu nitakuwa makini kwa usalama wa kila mmoja na taifa langu. Nitakuwa mzalendo. Naipenda nchi yangu. Anashangiliwa sana na anashuka jukwaani.

Mwanamziki
Anapanda jukwaani kwa mwondoko wa aina yake anashangiliwa anasema," mimi ni kioo cha jamii" ninatambua kulinda utamaduni, kuimba nyimbo zenye maadili na kuzingatia tafsida kwa watoto na watu wazima, nitaburudisha, nitaelimisha; afya, tutunze mazingira, ustawi wa jamii, upendo, maendeleo kwa ujumla, amani nitaisisitiza. Mavazi yangu na mienendo yangu nitahakikisha inaenda sambamba na sanaa na haivuki mipaka maadili kwa ajili ya watu wote na taifa langu, "naipenda nchi yanguuuuu" anamalizia na ananza kushuka huku akishagiliwa sana.

Kiongozi
Anashangiliwa sana, anaingia jukwaani anashika kipaza sauti, "taifa langu nchi yangu" watu wanaitikaa Mkuu! Mkuu! Mkuu! Kiongoziii! Anasema, hatamu ni kwa watu wangu! nitahakikisha amani, usawa, uzalendo na nitajitoa kwa ajili ya watu, nitakataa rushwa na nitafanya kazi zangu kwa bidii, sitapenda kukosea, nikikosea nitajiondoa madarakani hakika nitajiuzulu kwa ajili ya taifa langu. Watu wanamshangilia na anashuka jukwaani.

Mwongozaji
Anasimama na kusema taifa linasherehekea, sherehe hizi hazitakoma tutalipigania taifa letu kwa uzalendo mkubwa kila mmoja aahidi. Watu wanashangilia, Taifa! Taifa! Taifa! Watu wanaahidi wanaitika, taifa amani idumu!
 
Upvote 0
Back
Top Bottom