Maneno haya katika lugha ya kiswahili yanatumikaje na maana yake

Maneno haya katika lugha ya kiswahili yanatumikaje na maana yake

mathsjery

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2015
Posts
2,249
Reaction score
1,813
Nauliza tofauti na matumizi ya maneno haya nifahamisheni !

"Kijana" na "Binti"
 
Tofauti yake moja linamwakilisha -Me (Kijana) na +Ke (Binti)

Majina haya yote huelezea rika/umri kati ya 18-44
 
Najua binti maana yake ni msichana 'bikira' na kijana ni mwanaume alievuka miaka 18 lakini hajafikisha 40+
 
Binti maana yake ni " Mtoto wa kike wa"
Mfano: Binti Alli = Mtoto wa kike wa Alli.
Kijana ni mtu yeyote mwenye umri kati ya miaka 15-45. Neno kijana halihusiani na jinsia.
Neno linalohusiana na jinsia ni "mwana" ambalo lina maana ya "Mtoto wa kiume wa..."
Mfano: Mwana wa Daudi = Mtoto wa kiume wa Daudi.
 
Hapa inategemea na Imani kuna watu wengine huamini kwamba Binti ni mtu yoyote mwanamke na kijana ni mwanamme yoyotte kati ya miaka 18-30, wengine wanaona Binti ni aliekwisha vunja ungo hadi kuolewa tu na kijana ni ni yoyote akiwa mwanamke au mwanamme mwnye umri wa miaka 18-35
 
Hapo hakuna imani. kinachohitajika ni maana ya hayo maneno. Hata hivyo maana uliyotoa si sahihi.
 
Tofauti yake moja linamwakilisha -Me (Kijana) na +Ke (Binti)

Majina haya yote huelezea rika/umri kati ya 18-44
Umeteleza kidogo. Tofauti ya maneno hayo ni kwamba moja linaelezea rika na lingine linaelezea jinsia. Neno Kijana linaelezea rika. Neno Binti linaelezea jinsia ya kike.

Jinsia ya kiume inaelezewa na neno Mwana.
 
Hata kijana linaweza tumika kwa msichana.

Tunaposema vijana ni taifa la leo, hatumaanishi ni wakiume tu, hata ke
 
Kijana✓mtoto wa kiume(18-45).
Binyi✓mtoto wa kike amevunja ungo/kigori((14_35).
 
Back
Top Bottom