matawi ya juu: mtu wa kipato cha juu au kuwa na cheo
ATM: Hili neno ni kifupi cha Automated Teller Machine; Mashine inayo toa fedha na mara nyingi ukaa nje ya baadhi ya benki au Super market kwa ajili ya kutolea fedha na utumia kadi. Vile vile kwa lugha ya mtaani linatumika haswa kwa wanawake kuwaita wanaume wenye kuwaonga. Pia neno lingine ni (Buzi au kuchuna buzi)
kujiachia: Kwa kiswahili fasaha ni kuwa mzembe, kukaa bila ya kufanyakazi;
usipime: Kwa kiswahili cha mtaani ili neno lina maana ya usijaribu
adabu tupu: Kuwa na nidhamu
Kubambia: ......
mwana: Mtoto wa..., kwa lugha ya mitaani linatumika kwa watu ambao ni maswahiba (marafiki) tena wenye umri unao fanana.
Majita: Kabila linalopatikana Musoma (Jita... Mjita au Wajita). Kwa lugha ya mtaani ni Askari police au askari jeshi.
mwake: Kwa lugha ya mtaani maana yake ni kitu kizuri au kupatia jambo.
michosho: Kwa lugha ya mtaani maana yake ni mtu mwenye maneno ya kuchosha, mtu asiye makini
mkwanja: Kwa lugha ya mtaani maana yake ni kuwa na uwezo wa kifedha, Pesa
kichaa wangu: Kwa lugha ya mtaani maana yake ni rafiki yangu.
kumchomolea: kumkatalia.
kumpa sound: kumwongelesha mtu kwa ajili ya kupata kitu. lakini kwa njia ya uwongo.
Unanitega unanitaka: Haya ni maneno mawili tofauti, na mara nyingi yanaandikwa hivi;
Unanitega au unanitaka, na utumiwa na wanawake kuwauliza wanaume pale wanapotongozwa. Wakimaanisha kuwa 'unanitaka kwa ukweli au unaniongopea'
manjemanje: Sina uhakika na hili neno, lakini kama una maanisha
Manjee, kwa kiswahili chamtaani maana yake ni chakula
kupiga mkeka: Ni neno lenye kutumikwa kwa wanao kwenda Kusali msikitini, maana nyngine utumika mpirani wakimaanisha kusakata kabumbu kwa kutoleana pasi maridhawa.
kutia timu: maana yake ni kufuatilia jambo, kuingia sehemu bila kutegemewa au kualikwa.
manjemanje: Angalia hapo juu.
kumdakisha: Kumpa mtu kitu, kama vile pesa.
Nyomi: Kujaa na mara nyingi ili neno linatumika kwenye mabasi ya abiria. Au kwenye viwanja vya michezo (Mpira n.k)
Shalo tina tina: ....
aminia: Maana yake ni ...ndio ivyo ivyo... na mara nyingi utawasikia wakisema ...
aminia babake.
Mdosho: Mwanamke mrembo au msichana, ili neno limefupishwa kutoka neno
Kidosho.
Kama kawa: Kama kawaida.
full chaja: ....
serengeti girls/boy: Wavulana/Wasichana wenye kutembe na wanaume/wanawake wenye umri mkubwa.
kicheche: Mtu mwenye kupenda ngono na haswa linatumika kwa wavulana na wasichana wenye umri mdogo
Kama kutakuwa na makosa wapo wataalam watasahihisha.