Maneno haya ya Kiarabu yana maana gani katika nembo ya Zanzibar University ilhali lugha rasmi za taifa (Bara na Visiwani) ni Kiingereza na Kiswahili?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2012
Posts
15,892
Reaction score
16,476
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa JamiiForums.

Ndugu zangu Watanzania, eti;

Maneno haya ya kiarabu yana maana gani katika nembo ya "Zanzibar University" ilhali lugha rasmi za taifa (Bara na Visiwani) ni kiingereza pamoja na Kiswahili?

images.jpg

MAELEZO MACHACHE SANA KUHUSIANA NA "ZANZIBAR UNIVERSITY"
=========
The Zanzibar University (ZU) is a private university in Zanzibar, Tanzania. It opened in 1998 as the first university in Zanzibar, is a private university sponsored by the Darul Iman Charitable Association, an Islamic religious organization in Ontario, Canada. It is situated at Tunguu area, in the Central District, some 12 miles (19 km) from Zanzibar Town. The University campus, with a total area of 170 acres (0.69 km2) of land, is located among quiet countryside surroundings overlooking the Indian Ocean. There is public transport to the University.
=========

ANGALIZO/TAHADHARI: Ninaomba tuepeka kabisa comments za kisiasa, udini (uislamu na ukristo) pamoja na ukabila (uzanzibar pamoja na ubara) kwa maana sio lengo la mada hii.

Sisi watanzania wote ni ndugu na wamoja licha ya tofauti zetu chache (Minor Differences) na sote tuungane katika kutatua changamoto zetu za kitaifa ili tuweze kusonga mbele zaidi kwa manufaa ya vizazi vijavyo.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
People of Tanzania we should know that we are slaves in our own country, so the only opportunity we have now is to change the whole system by having our own powers.
 
Huko tuko sambamba na Maalim Seif kuukwaa uraisi, tusha Anza kuandika karamu
Nimesema hivi ndugu yangu;

ANGALIZO/TAHADHARI: Ninaomba tuepeka kabisa comments za kisiasa, udini (uislamu na ukristo) pamoja na ukabila (uzanzibar pamoja na ubara) kwa maana sio lengo la mada hii.
 
Mi naona maelezo uliyotoa yamejitosheleza umesema ni private’ university pia inafadhiliwa na organisation ya Dini. Hata hivyo Zanzibar ni makazi ya muda mrefu sana ya waarabu hata Tamaduni zao zinafanana kwa kiasi kikubwa mi sioni tatizo hapo ni diversity tu hapo
 
Hata hivyo Zanzibar ni makazi ya muda mrefu sana ya waarabu hata Tamaduni zao zinafanana kwa kiasi kikubwa mi sioni tatizo hapo ni diversity tu hapo
Kiarabu si lugha ya taifa (Bara na Visiwani)
 
Mi naona maelezo uliyotoa yamejitosheleza umesema ni private’ university pia inafadhiliwa na organisation ya Dini.
Dini kufadhili huduma za kijamii kama elimu hakika ni jambo jema sana na kwa kweli ninawapongeza kwa hili.
 
Kiarabu si lugha ya taifa (Bara na Visiwani)
Kuna baadhi sehemu nilikuta ni taasisi ya kulelea watoto Yatima ya kanisa katoliki bango lao limeandika kwa kilatini na chini limepitishwa maneno ya kingereza...Taasisi ya kichina confusius UDSM wameanza na Kichina wakamalizia na kingereza kwa hiyo hilo jambo sio geni
 
Taasisi ya kichina confusius UDSM wameanza na Kichina wakamalizia na kingereza kwa hiyo hilo jambo sio geni
Sio jambo geni sawa mkuu lakini je, ni jambo sahihi?

Alafu weka na supporting picture tuone tusiandikie mate na wino upo
 
Weka na picha kidogo tuone hayo maneno ya kiarabu pale Ikulu ndugu yangu
Kwaluwa sijawah kufika huko na sijui kama inaruhusiwa kuoiga picha kwa mtu asiye husika ila wadau wanasema maneno hayo yanasomeka.

ingieni kwa amani
 
Kuna baadhi sehemu nilikuta ni taasisi ya kulelea watoto Yatima ya kanisa katoliki bango lao limeandika kwa kilatini na chini limepitishwa maneno ya kingereza...Taasisi ya kichina confusius UDSM wameanza na Kichina wakamalizia na kingereza kwa hiyo hilo jambo sio geni
Hata visima vya maji au vituo vya watoto yatima vilivyo jengwa na waturuki mabango yao yameandikwa kwa lugha ya kituruki.

Sidhani kama kuna tatizo kwa Chuo kilichojengwa na taasisi ya dini (kiislam) kuwa na maandishi ya kiarabu kwasababu ndio taratibu zao za imani, hata misikiti mingi ina maandishi ya kiarabu japo kiarabu sio lugha ya taifa, na makanisa mengi ya katoliki (RC) utakuta maandishi ya kilatini japo kilatini sio lugha ya taifa.

Sijui maana yake lakini nahisi ndio hiyo ya jina la taasisi hiyo iliyojenga Chuo hicho!
 
Sio jambo geni sawa mkuu lakini je, ni jambo sahihi?

Alafu weka na supporting picture tuone tusiandikie mate na wino upo
Google tu Confucius UDSM wataleta picha by the way kua na lugha mbili za taifa haimaanishi nyingine zisitumike maana yake ni kwa kwa shughuli za kiserikali tu hasa mawasiliano ya maandishi au mdomo hizo ndio zitatumika
 
Maana yake ni nini?
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums.

Ndugu zangu watanzania eti;

Maneno haya ya kiarabu yana maana gani katika nembo ya "Zanzibar University" ilhali lugha rasmi za taifa (Bara na Visiwani) ni kiingereza pamoja na Kiswahili?

images.jpg

MAELEZO MACHACHE SANA KUHUSIANA NA "ZANZIBAR UNIVERSITY"
=========
The Zanzibar University (ZU) is a private university in Zanzibar, Tanzania. It opened in 1998 as the first university in Zanzibar, is a private university sponsored by the Darul Iman Charitable Association, an Islamic religious organization in Ontario, Canada. It is situated at Tunguu area, in the Central District, some 12 miles (19 km) from Zanzibar Town. The University campus, with a total area of 170 acres (0.69 km2) of land, is located among quiet countryside surroundings overlooking the Indian Ocean. There is public transport to the University.
=========

ANGALIZO/TAHADHARI: Ninaomba tuepeka kabisa comments za kisiasa, udini (uislamu na ukristo) pamoja na ukabila (uzanzibar pamoja na ubara) kwa maana sio lengo la mada hii.

Sisi watanzania wote ni ndugu na wamoja licha ya tofauti zetu chache (Minor Differences) na sote tuungane katika kutatua changamoto zetu za kitaifa ili tuweze kusonga mbele zaidi kwa manufaa ya vizazi vijavyo.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Maneno hayo maana yake ni

جامعة زنجبار : Chuo kikuu cha zanzibar

Yaani jaamiatu zin,jibaar _ chuo kikuu cha zanzibar.

Kama kusema kwa kiingereza UNIVERSITY.

Ndio maana kule arabuni saudia kuna chuo kinaitwa "JAAMIATU ISLAAMIYYAH" yaani "JAAMIATU " ile ile ya kule zanzibar.

Sasa hii "jaamiatu islamiyyah" maana yake ni islamic university yaani chuo kikuu cha kiislamu.
 
Back
Top Bottom