maneno "juice" na "i miss you" kwa kiswahili

juice ni SHARUBATI kwa Kiswahili sanifu
 
JF kwa kukopiana siredi bwana hamjambo!!!
 
Hapana, juice ni juisi na sherbet ndiyo sharubati.
Sasa sherbet kama unaijua si juice hata kidogo.
NN hapa ndipo nakubaliana na wewe kwenye uzi mmoja kwamba si lazima kutafsiri kila neno, Juisi inaeleweka hata kwa watoto
 
Alichokisema kichwat ni kweli tena kweli tupu. Juice ni neno la Kiingereza. Kiswahili chake kinachokubalika hata TATAKI ni sharubati. Aliye mbishi na aiendee Kamusi.
 
Alichokisema kichwat ni kweli tena kweli tupu. Juice ni neno la Kiingereza. Kiswahili chake kinachokubalika hata TATAKI ni sharubati. Aliye mbishi na aiendee Kamusi.

Sharubati ni sherbet. Unaijua sherbet wewe?

Nitafutie kamusi yoyote ya Kiswahili inayotafsiri juice kama sharubati.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…