Maneno machache kwako mtafutaji

Joined
Jun 8, 2016
Posts
83
Reaction score
652
Maneno machache kwako wewe ambaye dunia bado inakuweka chini,
Hawakujui,
Watafanya kila liwezekanalo kukufanya ubaki ulipo,
Watalipa polisi wakuweka ndani bila wewe kufanya kosa,
Watakutishia,
Watabadilisha maneno waliosema na kutumia nguvu zao kukuhutumu,
Wataongea juu yako bila kukupa nafasi ya kujitetea,
Watakuona we muizi bila wewe kuiba,
Watakupandisha hasira' na kweli jamani hasira hasara, ila ukitulia jua kwamba yatapita,
Jua kwamba wapo wengi wasio na uwezo wala nguvu na wanatafuta kama wewe ambao kila siku haya mambo yanawatokea,
Jua kwamba haya mambo yamewekwa kukubakisha wewe ulipo,
Jua kwamba wapo ambao wameshapitia hayohayo na leo mambo ni tofauti,
Jua kwamba dunia inajua, mbingu zinajua, miti inaona, wanyama wapaao angani wanaona ukweli..
Jua kwamba kesho inakuja..
Mkwanzania.
 
Dunia in mengi lakini hii itukae akilini wote ni kwamb ili uuone uzuri wa nyumba sharti uwe mbali nayo lakini ukiisogelea utakacho ishia kuon ni mlango tu
 
Ahahahaha
Yaaa fikiria hiyo kauli zeni iweke kwenye uhalisia wa hustle zetu za kila siku kuna wana wanatamani kazi yako wewe uliyo nayo lakini hawajui kuwa ni mambo mangapi wewe unakutana nayo na kuyavumilia katika iyo kazi yako bro the same tu kutoboa mkuu so vitu waga havipo kama tunavyoviona
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…