Maneno mapya yakiswahili nisiyovutiwa nayo...

Wapuuzi watakiua kiswahili. Kwanza tungekuwa na baraza la kiswahili la EA na ndilo lihusike kupitisha maneno. Si hawa wanaotaka kuonyesha uhodari wao wa kiswahili.
 
Hata wazee wa zamani wakati wakielewesha watu kuhusu sex waligundua mnapokutana hampaswi mmojawapo kumbana mwenzie.. hivyo ngono wakaiita kutom-bana .
duh!
 
Drone= ndege isiyo na rubani

Artificial intelligence= akili bandia
ndege isiyo na rubani ni maelezo sio jina!, mkuu drone zina rubani isipokuwa tu rubani wake hakai kwenye chombo.
 
Mpaka wakenya wanatuzidi khaaa.....
 
ipo siku tutakuja kuvamia hao akina bakita tukavuruge mule tutafune vitabu!, mambo gani haya au hawalipwi hivyo wanaamua kutuonyesha ufundi ktk namna nyengine..?🤣
TUKI pale UDSM wanafanya vyema sana.
 
Akili mnemba badala yake liwe AKILI BUNIFU
 
..siku hizi kumeibuka neno "hiko" badala hicho! Huwa nasikia kinyaa
 
Kuna maneno kibao mazuri mapya hawajayaweke kwenye kamusi mfano, kula bata, sepa, zingua.
Pia akili mnemba bora iitwe akili bandia,
 
nimechekasana magoti wasalimie nyegere hapo kisarawe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…