A. Mbuzi 1. Mnyama, 2. Kifaa cha kukunia nazi.
B. Kaa 1. la moto 2. Kuketi chini 3.Wadudu wa pwani
C. Tata 1. Mtoto anayeanza kutembea 2. Kitu chenye utata.
D. Buku (daftari) 1. Panya mkubwa 2. Buku /daftari la kuandikia.
E. Kutu 1. Kinyesi, 2 Kitu chenye asili ya chuma kuanza kuharibika.
F. Maziwa 1. Ya kunywa 2. Maumbo makubwa ya maji yaliyotuama 3. Matiti
G. Gongo 1. Ulevi 2. Gongo la mti.
H. Kifungo 1. Cha shati 2. Cha jela.
I. Taa 1. Kitu kitoacho mwangaza 2. Samaki wa baharini.
J. Kaa 1. La moto 2. Mdudu wa Pwani, 3. Kuketi chini.
K. Paa 1. La nyumba 2. Kupaa angani 3. Mnyama pori.
L. Mto 1. Wa kulalia 2. Umbo la maji yenye kutiririka.
M. Meza 1. Kumeza 2. Meza ya kuandikia / kulia.
N. Kulia 1. Muelekeo wa njia 2. Kulia kuonesha huzini n.k
Chap chap ni hayo tu mkuu.
Tanbihi, kuna yaandikwayo sawa ila hutamkwa tofauti na hapa ndipo utaipata ladha ya lugha.
I, J, K