Maneno tata

Ailars David

Senior Member
Joined
Jul 6, 2017
Posts
128
Reaction score
36
Wakuu uzi huu ni maalumu kwa ajili ya kujua maana mbalimbali za maneno tata.

Mfano:
KATA - Kata mti | Kata kiuno

Nipe neno na wewe lenye maana zaidi ya moja.
 
A. Mbuzi 1. Mnyama, 2. Kifaa cha kukunia nazi.
B. Kaa 1. la moto 2. Kuketi chini 3.Wadudu wa pwani
C. Tata 1. Mtoto anayeanza kutembea 2. Kitu chenye utata.
D. Buku (daftari) 1. Panya mkubwa 2. Buku /daftari la kuandikia.
E. Kutu 1. Kinyesi, 2 Kitu chenye asili ya chuma kuanza kuharibika.
F. Maziwa 1. Ya kunywa 2. Maumbo makubwa ya maji yaliyotuama 3. Matiti
G. Gongo 1. Ulevi 2. Gongo la mti.
H. Kifungo 1. Cha shati 2. Cha jela.
I. Taa 1. Kitu kitoacho mwangaza 2. Samaki wa baharini.
J. Kaa 1. La moto 2. Mdudu wa Pwani, 3. Kuketi chini.
K. Paa 1. La nyumba 2. Kupaa angani 3. Mnyama pori.
L. Mto 1. Wa kulalia 2. Umbo la maji yenye kutiririka.
M. Meza 1. Kumeza 2. Meza ya kuandikia / kulia.
N. Kulia 1. Muelekeo wa njia 2. Kulia kuonesha huzini n.k

Chap chap ni hayo tu mkuu.
Tanbihi, kuna yaandikwayo sawa ila hutamkwa tofauti na hapa ndipo utaipata ladha ya lugha.

I, J, K
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…