Maneno ya Ajabu.

uporoto01

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2008
Posts
4,698
Reaction score
1,423
Hivi mwanamme ana maana gani anaposema 'girlfriend wangu wa kike' au mwanamke anaposema 'boyfriend wangu wa kiume'.Maneno haya nakutana nayo kila mara kwenye mazungumzo na watu na nimechoka kuwasahihisha.
 
Inategemeana ni nani anayeongea!Kama ni mtu mwelewa, basi ujue ni utani, lakini kama ni huku kwetu uswazi ujue ndo kamaanisha hivyo, na umsahihishe bila kuchoka kwa nia ya kumsaidia!Pole!
 
Inategemeana ni nani anayeongea!Kama ni mtu mwelewa, basi ujue ni utani, lakini kama ni huku kwetu uswazi ujue ndo kamaanisha hivyo, na umsahihishe bila kuchoka kwa nia ya kumsaidia!Pole!

hiyo kweli ipo! wabongo inabidi tubadilike! mfano: my wife wangu! hahahahahahaha, your husband wako! kazi ipo!
 
..... Maneno haya nakutana nayo kila mara kwenye mazungumzo na watu na nimechoka kuwasahihisha.
Rafiki ukichoka upumzike tu! Waache! Ujue dunia inajaa ujinga na wewe u nani kuokoa dunia??
 
hiyo kweli ipo! wabongo inabidi tubadilike! mfano: my wife wangu! hahahahahahaha, your husband wako! kazi ipo!
Hapo umenena nilishawahi kumsikia mtangazaji wa Clouds FM akisema barabara ya ocean Road nilicheka sana.
 
Girlfriend wa kike, lol.

Pengine wengine wana ma girlfriend wa kiume.Huwezi kujua mambo ya siku hizi.
 
Labda ni katika manjonjo tu ya kuongea... ni sawa mtu aseme "Mai waifu wake" Wakati mwingine ni lugha za mitaani tu... maana hazina kanuni yoyote as long as wanaelewana hakuna tatizo... tatizo linakuja pale luha hizi zinapo ingia kwenye vyombo vya habari na kutumiwa na watu ambao tunatarajia wawe makini na kile kinacho toka vinywani mwao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…