"TUMERUHUSU Walanguzi na Wahujumu Uchumi kuongoza nchi. Wananchi wamefika mahali ambapo wanashindwa kutofautisha kati ya viongozi wa chama (CCM) na Serikali na Walanguzi na Wahujumu uchumi wa nchi."
Ilikuwa Machi 7, 1983 Dodoma.
Source: Raia Mwema
Maneno hayo yalisemwa na kiongozi mzalendo kabisa ambaye ameandika historia katika nchi hii ambayo ni vigumu kufutika vizazi hata vizazi,
Kipindi hicho walanguzi na wahujumu uchumi ni maneno yaliyotumika, kwa sasa tunaweza kusema Hayati Sokoine alikuwa anamanisha wezi au mafisadi kwa maneno yaliyozoeleka kwa sasa .
Swali la kujiuliza ni kwamba kumbe ufisadi ndani ya CCM na serikali ya CCM ni jadi yao miaka na miaka. Kama ni hivyo kwa nini tunaendelea kukipa chama hiki dhamana ya kuongoza nchi ?
Mimi nionavyo kwa sasa hali aliyokuwa akiikemea Sokoine kwa sasa ni mbaya kuliko wakati ule, Wako wapi viongozi wenye uzalendo wa kuweza kukemea mafisadi kutumia nguvu ya pesa kuingia madarakani na kisha baada ya hapo kuendelea kuliangamiza Taifa.
Kwa maneno hayo ya kiongozi wetu mpendwa nakiona kifo cha CCM kimekaribia , Watanzania tutafakari na kuchukua hatua .
Nawasilisha