Elections 2010 Maneno ya JK, Dr Slaa na Prof Lipumba 2010

Sir R

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2009
Posts
2,175
Reaction score
300
Zijue ahadi za wagombea nafasi ya Urais
Mgombea wa CCM Jakaya Kikwete, anaongoza kwa ahadi hizo baada ya kutoa ahadi kubwa zaidi 25 akifuatiwa na mgombea wa Chadema Dk Willbroad Slaa ambaye tayari metoa ahadi kubwa nane na Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF aliyetoa ahadi saba hadi jana.

Ahadi za Kikwete:
1. Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa.
2. Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi
3. Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi
4. Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba
5. Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma
6. Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda
7. Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa
8. Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu
9. Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino
10. Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba
11. Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali
12. Serikali kulisaidia vyama vya ushirika
13. Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu
14. Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani
15. Kulinda muungano kwa nguvu zote
16. Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa
17.Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa
18.Kujenga bandari Kasanga mkoani Rukwa
19.Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo
20.Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira
21.Kuzuia hatari za kisiwa cha Pangani kuzama
22.Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini

23. Tatizo la maji kuwa historia Tanga
24. Walimu kuwa na laptop
25. Kigoma kuwa Dubai ya Afrika


Ahadi za Profesa Lipumba:
1.Elimu ya bure kuanzia msingi hadi chuo kikuu
2.Kubana matumizi kwa kupunguza ukubwa wa baraza la mawaziri
3.Kuunda serikali shirikishi
4.Kusimamia rasilimali
5.Kuimarisha miundombinu
6. Kusimamia na kuboresha afya
7. Kuboresha kilimo, viwanda na uwekezaji

Ahadi za Dk Slaa:
1.Kujenga nchi isiyo na ufisadi
2.Kufufua Tanganyika ili irejee mezani kujadili muungano na Zanzibar
3.Kufufua uchumi wa nchi kwa kutumia rasilimali zilizopo
4.Kukata asilimia 20 ya mshahara wa rais
5.Kupunguza mishahara ya wabunge kwa asilimia 15
6. Kuweka Mwenge wa Uhuru Jumba la Makumbusho
7. Kutoa huduma bora za afya bure
8. kufuta kodi ya vifaa vya



My take
Ndiyo tunayoyahitaji haya?























 
umesahau hapo kwa Slaa. 9. Kila mtoto wa kitanzania lazima afike kidato cha sita kama elimu ya msingi. 10. Kuboresha michezo na utamaduni kwa kuendeleza makocha wazawa.
 
Imekuwaje mtoa thread amechuja inzi akameza ngamia.ahadi ya kwanza ni kubadili katiba,kufuta wakuu wa mikoa na wilaya, na kufumua mfumo wa elimu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…