OLS
JF-Expert Member
- Oct 12, 2019
- 426
- 685
Kuna suala sijui la majengo 70 kila jimbo, sijajua lilianzia wapi lakini Spika wa Bunge Job Ndugai amesema Majimbo hayana tafsiri nzuri kuna majimbo yana kata mbili, huku mengine yakiwa na kata hadi 15. Pia idadi ya watu katika majimbo ni tofauti, kuna majimbo hata watu laki moja hawafiki
Amesema Majimbo hayana maana nzuri kwa hiyo mgao wa hivyo vyumba utegemee idadi ya watu badala ya majimbo
Hoja yangu ipo kwenye sababu ya kuwa na majimbo au kuongeza majimbo. Hivyo ni vyema tuseme jimbo ili liwe jimbo inabidi liwe na watu wangapi hii itaepusha tabia ya kuongeza wabunge bila kuwa na sababu ya msingi.
Kwa sasa tuna wabunge zaidi ya 300 na mambo hayaendi, ni vyema kujua wastani wa watu ambao kila mbunge anawasemea badala ya kuwa na jimbo kisa mtoto wa mjomba hana kazi tunaanzisha ili apate sehemu ya kula
Ni muhimu pia kwa miliki nyingine za kiutawala kuwa na maana inayokaa kiuchumi, mathalani Mkoa, Wilaya nk ili tusiwe watu wa kuongeza mikoa na wilaya bila kuwa na maana bora ya kufanya hivyo
By the way mara nyingi wanasiasa wamekuwa wakisema wanafanya hivyo kusogeza huduma karibu kwa wananchi, hii ni hoja mfu... nitaeleza nikipata wasaa
Signed OEDIPUS