Maneno ya wana CCM hupinganana na matendo yao

Maneno ya wana CCM hupinganana na matendo yao

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
21,470
Reaction score
40,593
Chunga sana maneno ya wana CCM. Akisema haji jua anakuvizia aje kwa kustukiza. Maneno na matendo yao hupingana siku zote.

Waliposema Elimu Bila malipo ni jambo lisilowezekana, waliposhinda uchaguzi wakasema wanatoa Elimu bila ya malipo.

Wakisema kuwa wanataka nchi iwe na amani, wao humaanisha kuwa wanataka kuwagandamiza wapinzani wao kisiasa.

Walisema hela za ESCROW si za Umma lakini wakawakamta Kina Lugemarila kwa kuiba hizo hizo hela za Tegeta Escrow.

Wanasema CHADEMA ni chama dhaifu, lakini kila siku wanatamani wanachama wote wa CHADEMA wahamie CCM.

Walisema hawajui Lissu alipo, lakini mwisho wa siku wamemlipa mafao yake yote.

Wanasema chama chao ni cha kijamaa, lakini viongozi wake wengi ni Mabepari.

Wanasema viwanja vya mpira ni vyao, lakini wanachukua hela za umma kuvikarabati.

CCM hawaaminiki kabisa!!
 
Back
Top Bottom