Maneno yanayonichanganya

KASULI

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2020
Posts
599
Reaction score
677
Wadau lipi neno sahihi kati ya..

1. "Mbaka" au "Mpaka"

Mfano mtu aseme.....

"Mbaka sasa hakuna mshindi katika Pambano hili"

au

"Mpaka sasa hakuna mshindi katika pambano hili"

Yupi yuko sahihi hapo?


2. "Hembu" vs "Hebu"

Mfano:

"Hembu! Sogea nipite nikuoneshe"

Au

"Hebu! Sogea nipite nikuoneshe"


Kipi ni sahihi na kipi sioo Sahihi

Karibuni tujadilianeeee


Mara nyingi haya maneno yanatumiwa sana na Wakazi wa Dar Es Salaam na Maeneo ya Pwani
 
Wewe ni mtanzania? Au umejifunza kiswahili ukubwani??

Mpaka na Hebu.

Aisee, basi una mengi pia unakosea ila hayo mawili ndio umegundua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…