Mbele za mungu:
Katika lugha sayansi ya lugha wataalam wanatuambia kuwa kutumia wingi kwenye kumtaja Mwenyezi Mungu kunaitwa (Majestic or Royal Plural au wingi wa ukubwa na utukufu au wingi wa kifalme). Au kwa Kiswahili inajulikana kama Lugha ya Majazi. Majazi ni kule kutumia wingi kwa kumaanisha mtu au kitu kimoja... Hiyo yote ni katika kumtukuza Mwenyezi Mungu katika ufalme na dhati yake.
Tofauti ya Nabii na Mtume:
Nabii ni mjumbe aliyetumwa na Mwenyezi Mungu Aliyetukuka bila kuteremshiwa sheria au kanuni mpya ilhali Mtume ni yule aliyeteremshiwa sheria mpya. Hivyo, Nabii hutumia sheria ya Mtume aliyemtangulia.
Kwa ufupi ni kuwa kila Mtume ni Nabii lakini si kila Nabii ni Mtume. Mtume ana daraja kubwa kuliko Nabii.
Allahu yaalam