Mangi Meli (1866 - 1900)

Mangi Meli (1866 - 1900)

Manyanza

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
16,464
Reaction score
35,629
IMG-20240402-WA0019.jpg

Kiongozi wa Wachagga wa Old Moshi. Alinyongwa na Wajerumani kwa kukataa ukoloni, Wajerumani wakaondoka na fuvu lake, hadi leo hawajalirudisha.

Mangi Meli Kiusa, Alipambana na Wajerumani kwa kuwashinikiza waondoke katika himaya yake, jambo ambalo Wajerumani walilipinga kwa kudai kuwa baba yake Meli, ambaye alikuwa ameshafariki, ndiye aliyewakaribisha, hivyo hawawezi kuondoka.

Jambo lilizua mapambano makubwa na kupelekea kifo chake, ambapo aliuawa kwa kunyongwa na kisha kukatwa kichwa.

Chifu wa Marangu, aliyeitwa Mangi Marealle, na chifu wa Machame walikula njama na Wajerumani na kufanikiwa kumkamata Mangi Meli: walinzi wake wote walikubali kuajiriwa katika serikali ya Kijerumani, jambo lililorahisisha kukamatwa kwa Meli, kwani alibaki peke yake bila walinzi, hivyo walipovamia himaya hiyo hawakukumbana na changamoto yoyote.

Na alikuwa ametoboa masikio Mamangi walikua wakitoboa masikio hata Mangi wa wagweno Mangi Minja na yeye alikua ametoboa
 
Back
Top Bottom