Mangungu jiuzuru kuepuka aibu ya kung'olewa na wanachama

Mangungu jiuzuru kuepuka aibu ya kung'olewa na wanachama

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
Kwa takribani saa 48 sasa kuna mambo kibao yanaendelea ndani ya Simba.

Tajiri Mohamed Dewji ‘MO’ ameingia msituni mwenyewe. Ameamua kufumua kitu kimoja baada ya kingine kwa vitendo katika kuhakikisha Simba inakuwa moto wa kuotea mbali msimu ujao na kurejesha heshima ambayo imepoteza katika misimu mitatu mfululizo iliyopita.

Presha ya kujiuzulu inawakabili pia wajumbe wa bodi ya wakurugenzi akiwemo Mwenyekiti, Murtaza Mangungu ambao hawakuteuliwa na Dewji lakini kutokana na kutokuwa na mamlaka ya kikatiba,

Mpira huo umeachwa kwa wanachama kuamua wakati wa mkutano mkuu wa klabu hiyo. Upande huu wanachama walikuwa Seif Muba, Asha Baraka, Issa Masoud, Rodney Chiduo na Seleman Haroub na Mangungu.

1- Kama Mwenyekiti Mangungu anafahamu hana nguvu ya kuleta mabadiliko kwanini aendelee kubaki kwenye kiti?​

2- Kama Mwenyekiti Mangungu ndio Mwakilishi upande wa Wanachama mbona hajawahi kuja hadharani kusema yanayoendelea kwakuwa Wanachama ndio wanahisa wakuu?​

3- Katiba ya Simba inaruhusu Mkutano Mkuu wa dharura je amewahi kuitisha?​

4- Mpaka sasa Wanachama hawaridhishwi na mwenendo wa timu yeye kama Mwenyekiti kwanini yupo kimya? Ni labda apishe ama aje aseme na Wanachama timu inaendaje mbele.​

5- Kama Mwenyekiti amechukua hatua gani mpaka sasa kuhakikisha timu inadahili Wanachama wapya ili kuingiza mtaji wa sura mpya ndani ya timu?​

Yaani kivyovyote inaonesha hakuna sehemu Mwenyekiti Mangungu anaruka lawama kwakuwa 51% ipo upande wake na ndio wenye Simba yao, yaani Mashabiki ni sahihi kumlamu yeye.​

 
Ajabu punda wasiohusika ndio wameshikilia bango.Hayo yanahusu wanasimba na timu yao.Hao visunuku wengine katafuteni wa kuwakuna.
 
Ajabu punda wasiohusika ndio wameshikilia bango.Hayo yanahusu wanasimba na timu yao.Hao visunuku wengine katafuteni wa kuwakuna.
Tupo na Ngungus Boy mpaka pale atakapomaliza awamu yake,na tutamchagua tena.
 
Kwa takribani saa 48 sasa kuna mambo kibao yanaendelea ndani ya Simba. Tajiri Mohamed Dewji ‘MO’ ameingia msituni mwenyewe. Ameamua kufumua kitu kimoja baada ya kingine kwa vitendo katika kuhakikisha Simba inakuwa moto wa kuotea mbali msimu ujao na kurejesha heshima ambayo imepoteza katika misimu mitatu mfululizo iliyopita.

Presha ya kujiuzulu inawakabili pia wajumbe wa bodi ya wakurugenzi akiwemo Mwenyekiti, Murtaza Mangungu ambao hawakuteuliwa na Dewji lakini kutokana na kutokuwa na mamlaka ya kikatiba, mpira huo umeachwa kwa wanachama kuamua wakati wa mkutano mkuu wa klabu hiyo. Upande huu wanachama walikuwa Seif Muba, Asha Baraka, Issa Masoud, Rodney Chiduo na Seleman Haroub na Mangungu.

Habari za ndani ambazo nimezipata jana jioni ni kwamba huenda kukaibuka ombi la mkutano mkuu wa dharura muda wowote wiki ijayo kwani kuna wanachama wengi na wapenzi wa Simba wanashinikiza hilo.

Hata msajili vipi ,pambanieni nafasi ya pili na azam...ya kwanza hamtoipata kwa miaka hii miwili ijayo mfululizo.
 
Back
Top Bottom