“Mimi ndiye Mwenyekiti wa Simba Sc kwa kuchaguliwa na wanaofanya mabadiliko ni Wanachama wa Simba Sc na yapo matakwa kisheria yanayowalazimu kufanya hayo mabadiliko.
“Mkutano wa dharura una utaratibu wake wa kuitishwa, nilipokea barua kutoka Serikalini na nilivyopokea niliiwasilisha kwa Wajumbe wote wa Bodi kupitia kwa Mwenyekiti.
“Baadae nikamwandikia tena Barua nikamwambia kutokana na utekelezaji wa maelekezo ya Serikali nategemea kufanya mkutano August 2, akanijibu tarehe hiyo tunakusudia kufanya Marathon,” Mwenyekiti wa Simba Sc, Murtaza Mangungu akizungumza kwenye kipindi cha Radio cha Crown Sport.