Mangungu Simba sc hapamfai,Na Mashabiki Hawamuhitaji Mangungu.

Mangungu Simba sc hapamfai,Na Mashabiki Hawamuhitaji Mangungu.

mchawi wa kusini

JF-Expert Member
Joined
Apr 18, 2018
Posts
830
Reaction score
898
UCHAMBUZI WA ALICHOKIONGEA MANGUNGU CLOUDS
Wana Simba Msidanganyike na kurudi nyuma kwa maneno ya Ngungu.Kwanini
1.Kuenndelea kwake ni Mwendelezonwa visasi kwa wanachama
Jana tumemsikia wazi wazi akikana Tawi hadharani kwa sababu ya tofauti zake na mtu Mmoja unadhani lile tawi la VIP A ambalo lilizunduliwa kwa kkishindo hivyo wana jisikiaje jana ni makosa makubwa sana Je wewe ambalo ni tawi ulilokuwa unampinga mangungu Unadhani anawadhikiri aje ni chuki zinaendelea.Yapo matawi mengi yameonyesha kumpinga mangungu yasitegemee kukaa salama akiendelea kuwepo.

3.Ameendeleza na kuonyesha chuki wazi wazi na mashabiki Kitendo cha kuendelea kusema wanaompinga ni watu wa madaladala ni kudhalilisha mashabiki Pia kuusema watu wanachukia naye kwa sababu wana mpinga ni dhahiri anaendeleza mpasuko mkubwa ndani ya club na ana list yote ya wanaompinga Je unadhani hao mashabiki wataishije kwenye hiki kipindi chake ni wazi hawatakuwa na Amani wala huru NGUNGU AONDOKE.

3.Imani kwa wana Simba hawana imani na Ngungu tena.Ni wazi asilimia 95% hawana imani tena na Mangungu na wamejawa ha hofu.Mashabiki wa Simba kwa Sasa wana hofia kupelekwa polisi na club yao ambao wamejitolea kwa nguvu na pesa zao.Jana wana simba wanaendelea kuona kuwa kila wanachosema ni kutishiwa kukamatwa wana Simba hatujazoea hivyo Hivyo Mangungu anapaswa kuondoka kwa Kuleta Amani NGUNGU AONDOKE

4.Kitendo cha kusema kuwa Wanao mpinga hawana kadi ni kudhalilisha Mashabiki kwani kutokuwepo na kadi ni kosa lao au ni club.Amekoses mashabiki leo unawanyima fursa ya kuwa wanachama kisha unakwenda kuwasema hawana kadi Jamani kwa sababu hii ni Tosha NGUNGU AONDOKE

5.Mangungu ameshindwa kukanusha aliyoongea CPA Masoud na kusema kile kikao ni halali au si halali Ni wazi kuwa alibariki kile kikao Alipaswa kama kiongozi kutoa statement kuwa yale yalikuwa udhalilisho kwa mwekezaji wetu lakini hakuzungumzia chochote Ni wazi yuko naye.

RAI KWA WANASIMBA
Tumepiga kelele sana kuhusu Mangungu maneno aliyoongea jana ni kusema Mo ni jasiri ni MTEGO WA KUWALAGAI MASHABIKI.anachotaka mangungu huu upepo upoe waendeleze vita yao kama kawaida kwa hiyo msiingie kwenye huo mtego.
Alikuwa wapi mpaka haya yanatokea kwanini hakusema mpaka anaona wana Simba kutaka kumtoa TUSIDANGANYIKE MSIMAMO NI ULE ULE
TUKUTANE GWAMBINA
JUMAPILI SAA NNE ASUBUHI.
TUWASILISHE KILIO CHETU KWA RAISI WETU MAMA SAMIA SULUHU HASANI.
#Nguvu_moja💪🏻

Share iwafikie wengi Zaidi.

Twendeni Pamoja Wanasimba Kumuondoa Huyu Ngungu.
 
Back
Top Bottom