VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,137
- 17,908
Nafasi nachukua,shairi kukuandikia,
Albert Mangwea, uliyetangulia,
Asili ya Songea,mzaliwa wa Mbeya,
Mangwea tangulia!
Nilianza kukusikiliza,ili kukuelewa,
Mengi ukanifunza,hadi kunogewa,
Kwa zako stanza, zilizopangiliwa,
Mangwea tangulia!
Umeimba mambo mengi, kwa sanaa yatosha,
Tena yale ya msingi, UKIMWI kuelimisha,
MIMI ikawa shilingi, ujumbe kuufikisha,
Mangwea tangulia!
Kolabo ukafanya,na wenzako kukubali,
Wazembe ukawakanya, kwa lugha isiyo kali,
Utani ukaufanya, marafiki kila mahali,
Mangwea tangulia!
CNN na mikasi,nyimbo zako maarufu,
Zikakupatia nafasi, ya sanaa kali turufu,
Bila wasiwasi, hakuna uliyemkashifu,
Mangwea tangulia!
Kifo chako ugenini, funzo kubwa kwetu,
Ulikuwa safarini, kupigania wako utu,
Mengi sasa redioni, ulivyokutwa mfu,
Mangwea tangulia!
Pole kwa wazazi,ndugu na jamaa,
Pengo li wazi, marafiki wanashangaa,
Sasa tunayo kazi, kumpata anayefaa,
Mangwea tangulia!
Sisi tulikupenda, Mungu amekuhitaji,
Mema mengi umetenda, nje na ndani ya jiji,
Free-style ulipenda, kilikuwa chako kipaji,
Mangwea tangulia!
Mapungufu hukukosa, ni ubinadamu,
Hukuweza kutuasa, hatuwezi kulaumu,
Tunasamehe tangu sasa, na hilo ndilo muhimu,
Mangwea tangulia!
Lala salama Albert Mangwea! See you there my son!
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam.
Albert Mangwea, uliyetangulia,
Asili ya Songea,mzaliwa wa Mbeya,
Mangwea tangulia!
Nilianza kukusikiliza,ili kukuelewa,
Mengi ukanifunza,hadi kunogewa,
Kwa zako stanza, zilizopangiliwa,
Mangwea tangulia!
Umeimba mambo mengi, kwa sanaa yatosha,
Tena yale ya msingi, UKIMWI kuelimisha,
MIMI ikawa shilingi, ujumbe kuufikisha,
Mangwea tangulia!
Kolabo ukafanya,na wenzako kukubali,
Wazembe ukawakanya, kwa lugha isiyo kali,
Utani ukaufanya, marafiki kila mahali,
Mangwea tangulia!
CNN na mikasi,nyimbo zako maarufu,
Zikakupatia nafasi, ya sanaa kali turufu,
Bila wasiwasi, hakuna uliyemkashifu,
Mangwea tangulia!
Kifo chako ugenini, funzo kubwa kwetu,
Ulikuwa safarini, kupigania wako utu,
Mengi sasa redioni, ulivyokutwa mfu,
Mangwea tangulia!
Pole kwa wazazi,ndugu na jamaa,
Pengo li wazi, marafiki wanashangaa,
Sasa tunayo kazi, kumpata anayefaa,
Mangwea tangulia!
Sisi tulikupenda, Mungu amekuhitaji,
Mema mengi umetenda, nje na ndani ya jiji,
Free-style ulipenda, kilikuwa chako kipaji,
Mangwea tangulia!
Mapungufu hukukosa, ni ubinadamu,
Hukuweza kutuasa, hatuwezi kulaumu,
Tunasamehe tangu sasa, na hilo ndilo muhimu,
Mangwea tangulia!
Lala salama Albert Mangwea! See you there my son!
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam.