"Manipulated Man" kiatabu cha Ester Vilar. Je, umekisoma?

"Manipulated Man" kiatabu cha Ester Vilar. Je, umekisoma?

Natoa heshima zangu kwa wote waliopo katika jukwaa hili la JamiiForums. Kwa miaka mingi nimejikuta nikipata maarifa na ujuzi wa kutosha kupitia jukwaa hili (Jforums).

Nimefanikiwa kupata maarifa mbalimbali na nimevutiwa na bado ninavutiwa na namna ambavyo members wa JF wanavyowasilisha mambo yao. Uandishi wa nyota tano wa JBourne8, kudadavua facts kwa Da Vinci, mada za kukera na kujenga za Mtibeli, uandishi wa aina mbalimbali unapatikana hapa hapa.

Sina uwezo mkubwa wa kuandika kama hao members niliowaandika hapo juu ila ninatamani kuongea nanyi kuhusu kitabu nilichokisoma ndani ya hizi siku mbili tatu. Kitabu kinaitwa "Manipulated Man" na kimeandikwa na Ester Vilar, huyu Ester ni mwanamke ila ameshusha nondo nzito mno. Sijui kilimkumba nini (mwandishi) ila alichoandika kimenifanya nibadili mtazamo.

Kwa vizazi hivi vya karibuni ambavyo watoto wa kiume wanakosa malezi ya kiume na kujua namna ya ku-handle vitu kiume na namna sahihi ya kusimama nina recommend vijana wakiume wasome kitabu hiki.

Nikipata muda nitaandika summary fupi na kudodosa mambo machache niliyokumbana nayo huko. Kwa muda huu nita"attach" screenshot moja.

🐬
Kisogeze hapa hicho kitabu mkuu.
 
Pdf za vitabu zinapatikana web gani?
 
Ahsante kwa kuchangia

Mkuu anza kutupia summary kuhusu maana ya mwanaume na ukimaliza elezea maana ya mwanamke .

Then tuanze kuchambua

Ili tukichambue hiki Kitabu tutaangalia maeneo muhimu tutaangalia swala la ngono ambavyo hutumika kuwalaghai wanaume .

Sex as a reward .

Hapa tutaangalia kuwa wanaume wamekuwa manipulated kwa kuamini sex ni malipo kutokana kwa mwanamke aliyakuwa in fact mwanamke hutamani kufanya ngono the same mwanaume.

So karibu uanze uchambuzi then Mimi ntaendelea na kuandaa nondo .
 
Back
Top Bottom