KERO Manispaa ya Kinondoni mnapango gani na stendi ya Tegeta Nyuki? Mbona kama imetelekezwa hivi

KERO Manispaa ya Kinondoni mnapango gani na stendi ya Tegeta Nyuki? Mbona kama imetelekezwa hivi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Nimeona miaka ikienda lakini stendi ya Tegeta Nyuki ambayo ni moja ya stendi kubwa tu inayobeba magari mengi yanayofanya safari zake maeneo mengi katika Jiji hili la Dar es Salaam.

Kwa mfano kuna magari ya Tegeta Nyuki Makumbusho, Tegeta Nyuki - Simu 2000, Tegeta Nyuki - Bunju Sokoni, Tegeta Nyuki - Mbezi, Tegeta Nyuki Kivukoni nk. Sasa stendi hii kiukweli mazingira yake si rafiki na pindi mvua ikinyesha ndiyo tabu tubu kwa wasafiri na magari yenywe.

Soma Pia: Wafanyabiashara Soko la Tegeta Nyuki walalamikia ubovu wa miundombinu na mazingira machafu

Na stendi hii ndani yake kuna biashara mbalimbali zinafanyika zikiwemo za vyakula hata usafi wake si mzuri , Ukikaa kidogo utapigwa na vumbi kali kweli kwa sababu standi hiyo ni ya kidongo tu.

Embu wenye mamlaka husika fanyeni kweli kuitengeneza stendi hii ili mazingira yake yawe rafiki.

Untitled.jpg
Untitled56.jpg

 
Hapo picha n wakatii wa jua linawakaa...nendaa wakatii wa mvuaa mkuu n vichekeshoo
 
Back
Top Bottom