Katibu mkuu/Tamisemi
Dodoma
s.l.p
Dar es Salaam
YAH . KUMLALAMIKIA AFISA ELIMU WA SHULE ZA MSINGI MANISPAA YA MOSHI KWA JINA (D. BIMBALIRWA)
· Kwa kweli imebidi sasa waalimu wa manispaa ya moshi tuanze kupaza sauti zetu kwa namna yeyote ile iwayo hadi hapo tume huru ya uchunguzi itakapokuja hapa moshi kumchunguza huyu afisa elimu msing wa manispaa ya moshi.
· Sasa ni upendeleo kwa baadhi ya walimu anaowataka
· Ngono mtindo mmoja njooni shule ya msiingi J. K nyerere, muoneni kwa macho
· Shule za msing rau, na sokoine wakuu wa shule wanabadilishwa kama karata. Ukaguzi ulifika shule ya msingi sokoine na waligundua mkuu wa shule hana uwezo wa kuongoza, kioja ni kwamba afisa elimu alimwamisha mkuu huyo wa sokoine ambaye shule yake ilikuwa inapumulia mashine akambadilisha na mkuu wa shule ya rau. Sasa sijui anataka shule ya msingi Rau nayo ikafe tena au?.
· Afisa elimu amekuwa anachangisha waalimu wakuu michango ili ambayo anaitumia kujengea nyumba yake. nyumba anayoijenga ni kubwa sana na ipo maeneo ya msaranga (tume ichunguze kipato chake na kama ana mkopo benki ili ione maajabu ya nyumba hiyo/tumechoka kuchangishwa wakati sisi wengine hata kiwanja hatuna).
· Mbadhirifu wa mali za umma. Amegeuza kituo cha walimu mawenzi kuwa tuitisheni center, kituo ni kwa ajili ya walimu kujiendeleza inakuwaje anafanya kituo tuitisheni center. Ombi letu tunaomba kamati maalum ije kuchunguza malalamiko yetu. Huyu ni mbaguzi,mfanya kazi kwa kusikiliza maneno ya pembeni, asiye tenda haki, mla rushwa, mpenda ngono. KAMA HATUA HAZITACHUKULIWA STAHIKI TUTAMWANDIKIA WAZIRI WA ELIMU BARUA AFUATILIE YEYE
Nakala · Katibu mkuu/wizara ya elimu dar es salaam
· Ofisi ya waziri mkuu na serikali za mitaa
· Mkuu wa mkoa kilimanjaro
· Mkurugenzi wa manispaa ya moshi
· Ofisi TAKUKURU kilimanjaro