KERO Manispaa ya Singida iangalie Dampo la Msufini, linatunzwa vibaya na ni hatari kwa Afya

KERO Manispaa ya Singida iangalie Dampo la Msufini, linatunzwa vibaya na ni hatari kwa Afya

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Mliogwa

Member
Joined
Jun 6, 2024
Posts
37
Reaction score
37
Eneo la Msufini, Manispaa ya Singida ni mashughuli na maarufu kwa biashara hapa Singida. Shughuli nyingi za biashara za aina mbalimbali zinafanyika karibia eneo lote la Msufini.

Kinachosikitisha ni dampo lililopo katikati ya eneo hili likiwa limezungukwa na biashara ikiwemo za vyakula, bucha wauza mbogamboga n.k.

Dampo hili linajaa sana....uchafu hadi barabarani...harufu ni kali na usalama wa bidhaa za vyakula haswa mama lishe na bucha ni hatari sana kwa afya yetu.

Msimu wa mvua unakaribia hali itazidi kuwa mbaya. Bwana Afya Manispaa shughulika na dampo hili chukueni hatua km.

Mlivyoamua kufunga dampo la Soko Mjinga na Karakana mnapswa kufanya hivyo kwa soko hili la Msufini.

Pia soma ~ Dampo la Msufini hatimaye limesafishwa, mazingira sasa yamekuwa masafi

Snapchat-1034274300.jpg
Snapchat-1217162884.jpg
20241103_182519.jpg
20241103_182625.jpg
 
Back
Top Bottom