Pre GE2025 Manispaa ya Singida yaadhimisha siku ya Wanawake kwa bonanza na ugawaji gesi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

upupu255

Senior Member
Joined
Sep 4, 2024
Posts
119
Reaction score
144
Halmashauri ya Manispaa ya Singida, ikiongozwa na Mkurugenzi wake, Joanfaith Kataraia, imefanya bonanza maalum la kusherehekea Siku ya Wanawake. Katika bonanza hilo, yamefanyika mashindano ya kupika na kuchoma nyama pamoja na michezo mbalimbali.

Aidha, mitungi ya gesi 35 iligawiwa kwa mama lishe wote walioshiriki mashindano hayo na kwa wanaume waliochoma nyama, kama sehemu ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia pamoja na kulinda mazingira na afya za wananchi.

Mgeni rasmi kwenye bonanza hilo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Singida, Godwin Gondwe, ambaye amewahamasisha wanawake na wanaume kuendelea kutumia nishati safi ya kupikia ili kuunga mkono ajenda ya Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ya kulinda mazingira.

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Katika hatua nyingine, Mkurugenzi Joanfaith Kataraia amesema kuwa halmashauri hiyo inaendelea na maadhimisho ya Wiki ya Wanawake kwa kufanya matendo ya huruma kwa watoto wa Shule ya Tumaini Viziwi, Manispaa ya Singida.

Watoto hao wamepokea magodoro, mafuta na vitu vingine muhimu, na ugawaji huo uliongozwa na Mkuu wa Wilaya, Godwin Gondwe, pamoja na viongozi wengine.




CHANZO: Jambo TV
 
Gesi ikiisha mnawajazia au 😄

Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…