Manji Mwenyekiti Mpya Yanga!

KING COBRA

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2011
Posts
2,782
Reaction score
875
Taarifa Kutoka Ukumbi Wa Diamond Jublee Zinaonyesha Kuwa Yusufu Manji ameshinda nafasi ya Mweyekit timu ya Yanga:

Dalili hii ya Wapiga kura kuangalia pesa ya Rushwa ndiyo inaweza kuwaingiza akina Lowasa wenye mapesa hayo katika Madaraka!!!!!!!!!

Matokeo Kamili

Nafasi ya Mwenyekiti:
Yusuf Manji (kura 1876) 97.0%, John Jembele (kura 40) 2.6%, Edgar Chibura (kura 4) 0.24%

Nafasi ya Makamu Mwenyekiti:
Clement Sanga (kura 1948) 62.6%, Yono S Kevela (kura 475) 23%, Ayoub Nyenzi (kura 288) 14%

Nafasi ya Ujumbe:
Abdallah Bin Kleb (kura 1942), Moses Katabaro (kura 1068), Aaron Nyanda (kura 922), Geroge Manyama (kura 682), Beda Tindwa (kura 391), Edgar Fongo (kura 295), Graticius Ishengoma (kura 247), Jumanne Mwamenywa (kura 251), Justine Baruti (610), Lameck Nyambaya (kura 425), Omary Ndula (kura 170), Peter Haule (441), Ramadhan Said (249), Yono Kivela (123)

kutokana na matokeo yalivyo hapo juu safu ya viongozi waliochaguliwa ni
Mwenyekiti: Yusuf Manji,
Makamu Mwenyekiti: Clement Sanga
Wajumbe: Abdallah Bin Kleb, Moses Katabaro, Aaaron Nyanda, Geroge Manyama
 
Aangalie asijekimbizwa kama MENGI alivyokimbizwa yanga!watanzania tumeshindwa kujitawala mpaka mhindi anatutawala sasa yanga
 
Hata mimi ntakuwa Mwanachama wa Yanga sasa:eek2:
 
Reactions: SG8
Ngoja tuone pesa inavyocheza soka sasa!
 
Sitta shabiki wa Simba ulitarajia afurahie mafanikio ya Yanga? Usilete siasa kwenye michezo wewe tuambie Manji ameshinda kwa kura ngapi? Kama walijua hilo walifanya nini kuzuia asipite? Simple minded
 
Aangalie asijekimbizwa kama MENGI alivyokimbizwa yanga!watanzania tumeshindwa kujitawala mpaka mhindi anatutawala sasa yanga
Mbona Makocha tunatumia wazungu? Hivi Dewji sio Mhindi? Au wewe ulikuwa hujazaliwa wakati Kassim na Azim Dewji wakitawala Simba? Wabunge kibao wahindi na Waarabu wanatamba Bungeni kina MO, Murji, Abood, RA n.k leo Yusuph Manji ndio tatizo? Hata yule M/kiti wa SSC si Mwarabu? We vipi bwana?
 
Aangalie asijekimbizwa kama MENGI alivyokimbizwa yanga!watanzania tumeshindwa kujitawala mpaka mhindi anatutawala sasa yanga
wewe vipi...un ajua mpira au unaleta siasa za kila chama fulani ?ambao mhindi mbaya lakini kiatu chake dawa? sabodo ?

football haitaki mambo ya ubaguzi , hujaangalia euro juzi juzi tu namna ubaguzi ulivipigwa vita?
hujamuona John TERRY alipandishwa kizimbani kujibu tuhuma za ubaguzi? kama Yanga wangemwacha Manji kwa sababu za ubaguzi basi yanga ingeweza kufungiwa na fifa.
nadhani uchaguzi ujao 2015 kuna haja ya kupata Rais mhindi au mwarabau..tuone hali itakuwaje? naamini tutakuwa mbali zaidi....
 
Sitta shabiki wa Simba ulitarajia afurahie mafanikio ya Yanga? Usilete siasa kwenye michezo wewe tuambie Manji ameshinda kwa kura ngapi? Kama walijua hilo walifanya nini kuzuia asipite? Simple minded

naunga mkono hoja
 
 
Mkuu vip kuhusu nafasi zile zingine za makamu mwenyekiti?
 
Hongera manji,tunataka uige mfano wa huyu tajiri wa congo uifanye yanga iwe kama hivi....ili matajiri wengine wenye mapenzi na timu nyingine nao waige mfano wako na hatimae kuleta maendeleo kwenye club zetu





Sehemu ya Kupumzikia wakuu
View kutoka sehemu ya juu ya VIP
Moise Katumbi akiangalia uwanja viti vya mzunguko
Makabati ya kuwekewa nguo vyumba vya kubadilishia


Picha zote kwa hisani ya Mtandao wa TP Mazembe
 
Mkuu ingetosha tu kutuhabarisha sasa ukiweka zaidi maoni na msimamo wako unaondoa utamu wa habari yenyewe tena ukiwa kama mtoa hoja...au ndo yale ya kutoa na kuunga mkono hoja??...
 
Aangalie asijekimbizwa kama MENGI alivyokimbizwa yanga!watanzania tumeshindwa kujitawala mpaka mhindi anatutawala sasa yanga

Chelsea ni Timu ya Waingereza lakini Inafadhiliwa na Mrusi.
 

Kilichobaki kwa Manji ni kuoa dada zao wanachama wote wa Yanga ikiwa pamoja na Mashabiki wao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…