Manji ndiye aliunda genge la kumlilia lilia arudi Yanga

Chukwu emeka

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2018
Posts
24,314
Reaction score
38,919
Habari wanaJF,

Yanga timu yangu pendwa kabisa imekuwa ikipitia kipindi kigumu kwa takribani msimu mmoja na nusu hivi tangu uongozi uanze kuyumba na kupalaganyika,timbwili lilianza baada ya Yusuph Manji kujiuzuru na aliyekuwa kaimu mwenyekiti Clement Sanga kuchukua nafasi.Timu ilimuelemea Sanga na kushindwa kabisa na yeye akajiuzuru pamoja na baadhi ya wajumbe akiwemo Salum Mkemi.

Nimzunguzie Manji, huyu jamaa inaipenda na anataka kuiendesha Yanga ila njia anazotumia nizakitoto mno,anataka aipate Yanga kama mtu aliyebembelezwa na mwokozi kiasi kwamba anatengeneza magenge ya watu wanaopiga kelele kuonyesha wanamtaka Yanga, ili aipate kirahisi,baada ya kuona mission imefail ameamua kuandika barua ya kurudi Jangwani,binafsi naomba tusirudi nyuma tuendelee na utaratibu wa uchaguzi na Manji akitaka akachukue fomu apambane nawenzake kina Tarimba na si kuleta ujanja ujanja tu.

Wanayanga tunahitaji mabadiriko,tuache kurudi nyuma
 
Manji anaendelea kuwa mwenyekiti..lije jua au inyeshe mvua..Huyo mzee Akilimali katiba haimtambui hakuna baraza la wazee hiyo ni heshima tu waliyopewa...
 
hata wakati ule anagombea udiwani mbagala aliunda kundi la kumlilia waswahili njaa kali
 
Reactions: Tui
Katika makombe 29 ya ligi Manji kachukua mangapi?
Dunia ya wakati ule si ya sasa. Kikubwa, wana Yanga wataamua wenyewe sio mamluki
Achana na mambumbu utapoteza muda tu kuyajibu usidhani Msomali wao aliyewaita hivyo alikosea
 
Tatizo kila mwanasimba sasa hivi anajifanya ni Yanga ili tuu avuruge Manji asirudi.
 
Achana na mambumbu utapoteza muda tu kuyajibu usidhani Msomali wao aliyewaita hivyo alikosea
Sasa wana Msomali mwingine pale TFF imekuwa shida. Akisaidiwa na Mrundi imekuwa kama vita vita fungia fungia. Wamepata kibaraka mmoja anaitwa Mbwelambwela imekuwa wanafungia kila mtu.
 
Acha ushamba wewe. Unajua Kwanini Clement Sanga aliondolewa na TFF kuwa mwenyekiti wa bodi ya ligi?
Ni kwasababu TFF walitambua kurudi kwa Manji kwenye uenyekiti. Sasa unaongea nini hapa. Kibaraka wa simba wwe???
Mxy@*€#qx&>$.....
 
Sasa wana Msomali mwingine pale TFF imekuwa shida. Akisaidiwa na Mrundi imekuwa kama vita vita fungia fungia. Wamepata kibaraka mmoja anaitwa Mbwelambwela imekuwa wanafungia kila mtu.
Ndiyo yanataka yasimamie uchaguzi yaweke mapandikizi
 
Acha ushamba wewe. Unajua Kwanini Clement Sanga aliondolewa na TFF kuwa mwenyekiti wa bodi ya ligi?
Ni kwasababu TFF walitambua kurudi kwa Manji kwenye uenyekiti. Sasa unaongea nini hapa. Kibaraka wa simba wwe???
Mxy@*€#qx&>$.....
Najua ndiyo,shida wana Yanga wengi mnahisi kama bila Manji hakuna Yanga,hatumuhitaji mtu tunahitaji taasisi, siyo ujinga ujinga tu wa kulialia nayeye ni binadamu what if akifa na Yanga itakufa? Tangu ameondoka timu ingekuwa taasisi ingeyumba hadi kuchangishana? Tulio kwenye matawi kiasi fulani tumeipush timu kwa vimichango jambo ambalo ingekuwa taasisi tusigefikia huko.
 
Jibu swali.
Huna hela
Huna mpango wowote wa kuinusuru klabu
Hauna hata kadi ya uanachama
Huchangii cho chote kwenye timu.
Unaleta maneno kwenye pesa, acha ukuda binti
Kabisa, hapo swala ni kisu, kisu ndiyo kila kitu, wanachama sawa, ila soka la kileo ni kisu kama Waaarabu wa Man City, PSG n.k.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…