Manji sio Mungu Yanga Fungukeni wana Yanga

moodykabwe

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2015
Posts
625
Reaction score
602
YANGA IKISHUSHWA DARAJA, BOSS WETU, MWENYEKITI WETU NA MPANGAJI WETU ATAWAJIBIKA NA HAWEZI KUKWEPA KIKOMBE HIKI :

Daniel Naftal Ngogo :

Dr Jonas Tiboroa alifukuzwa na bwana mkubwa Ukatibu mkuu wa Yanga kwasababu eti alisafiri kwenda Kwenye seminar nchini Ghana bila ruhusa ya bwana mkubwa mbali ya ukweli kuwa Seminar ilikuwa na manufaa ya timu bado bwana mkubwa hakujali lakini pia pamoja na weledi mkubwa na utendaji uliotukuka wa Dr Tiboroa (Mhadhiri mwandamizi toka Chuo Kikuu cha Dar es salaam) bado alifukuzwa!!

-Siku Chache baada ya Dr Tiboroa kufukuzwa tukaja kuambiwa Yanga walishindwa kushiriki kikao muhimu sana cha maandalizi ya hatua ya makundi ya michuano ya Shirikisho, kikao ambacho kilikuwa kinajadili mambo muhimu kwa manufaa ya timu kama vile Udhamini wa jezi, haki ya matangazo (TV rights) pamoja na kanuni mbali mbali za mashindano, tukaishia kuzuiliwa kuvaa hata jezi zetu tulizo Kwenda nazo na kwa huruma tukasaidiwa na TFF kupata jezi zinazocomply na mashindano bado tukiporudi home tukaanza ugomvi wa kijinga wa haki ya kurusha mechi zetu wakati mambo yote yaliamliwa na kupitishwa na kikao cha Shirikisho la mpira Afrika ambacho hatukushiriki kwa uzembe wetu wenyewe.

-Leo tena dirisha la Usajili limefungwa, Yanga hawajawasilisha usajili wao TFF, usajili unaofanywa kupitia mfumo wa kisasa kupitia online application system maarufu kama 'TMS' (Transfer Merging System) , kwa mujibu wa TFF Yanga walipo alikwa Kwenye seminar ya Mafunzo ya namna Transfer Merging System inavyofanya kazi hawakupeleka muwakilishi, yaani mpaka Toto Afrika, Lipuli, Majimaji waliona umuhimu wa Mafunzo hayo Yanga hawakuona umuhimu wa kushiriki, nimesikiliza utetezi toka kwa kaimu katibu mkuu wa Yanga Baraka Desderbit amesema wao hawakushiriki kwasababu yeye hakuwepo na Jerry Muro alikuwa amefungiwa kwahiyo walikosa mtu wa kumpeleka kule Kwenye Mafunzo... hili ndio sababu ya Yanga kushindwa kushiriki Mafunzo haya muhimu kwa timu:kwakweli nimesikitika Sana kusikia utetezi huu Moja ya utetezi dhaifu na wa kijinga kabisa kuwahi kutolewa na Katibu Mkuu wa timu kama Yanga.

*MY TAKE *
-Toka Dr Tiboroa anafukuzwa na Manji timu imepwaya Sana Kwenye eneo la utendaji (Ofisi ya katibu mkuu) inashindwa kufanya kazi zake kikamilifu hata zile ndogo za kawaida ambazo hata timu za Lipuli FC toka Iringa zinatuzidi.

-Kaimu katibu mkuu wa Yanga Baraka Desderbit, Muhasibu huyu kitaluma toka Quality group, kijana mwenzetu hana uwezo wa kuwa katibu mkuu wa Yanga matukio haya yanayotokea Sasa ni ushahidi tosha kuwa boss wetu wa Secretarieti hatoshi, ni kweli wenda alikuwa Muhasibu mzuri pale Quality Group lakini Kuna utofauti mkubwa Kati ya kuendesha timu na kuwa Muhasibu wa kampuni binafsi.

-Washabiki wa Yanga tupunguze kumpigia makofi Manji kwa kila kitu anachosema tumfundishe kumkatalia na kusema hili sawa Lakin hili hapana bila hivyo atatupeleka shimoni.

-Mwisho boss wetu mkubwa tuliye mkodisha timu anapaswa kujua Yanga ni timu yenye umasikini mkubwa wa fedha lakini yenye utajili mkubwa Sana wa Mashabiki na wapenzi.. Kwa hiyo pesa sio kila kitu Kwenye timu, timu pia zinahitaji uongozi bora na Manji sio kiongozi bora wa timu bali ni mfadhiri bora hivyo anapaswa kupata katibu bora kama Dr Tiboroa,

Daniel Naftal Ngogo
Shabiki na mwanachama wa Yanga
 
Yanga wanafanya mambo kienyeji sana pale yanga inabidi wamapate Baraka Kizuguto ambaye kwa sasa ni meneja WA mashindano na TMS pale TFF ashike mite go cha meneja WA timu pale hayo mambo ya TMS na usimamizi WA timu yawe kwako maana yule Dogo yupo vizuri ana coz 3 za FIFA mambo ya TMS na umeneja afu yule ni yanga damu
 
Kula like mkuu dogo hata kipindi kile yupo yanga tovuti ya yanga ilikuwa update daily! Toka kaondoka yanga haipo digital media sijui hata kama tovuti inafanya kazi! #Kizuguto#rudi#Yanga#
 
imeishakufa zamani sana enzi zile hata livestream za mechi za uturuki alikuwa akitupa yaan yanga ibarudi nyuma sana baadhi ya mambo
 
YANGA IKISHUSHWA DARAJA, BOSS WETU, MWENYEKITI WETU NA MPANGAJI WETU ATAWAJIBIKA NA HAWEZI KUKWEPA KIKOMBE HIKI :

Daniel Naftal Ngogo :

Dr Jonas Tiboroa alifukuzwa na bwana mkubwa Ukatibu mkuu wa Yanga kwasababu eti alisafiri kwenda Kwenye seminar nchini Ghana bila ruhusa ya bwana mkubwa mbali ya ukweli kuwa Seminar ilikuwa na manufaa ya timu bado bwana mkubwa hakujali lakini pia pamoja na weledi mkubwa na utendaji uliotukuka wa Dr Tiboroa (Mhadhiri mwandamizi toka Chuo Kikuu cha Dar es salaam) bado alifukuzwa!!

-Siku Chache baada ya Dr Tiboroa kufukuzwa tukaja kuambiwa Yanga walishindwa kushiriki kikao muhimu sana cha maandalizi ya hatua ya makundi ya michuano ya Shirikisho, kikao ambacho kilikuwa kinajadili mambo muhimu kwa manufaa ya timu kama vile Udhamini wa jezi, haki ya matangazo (TV rights) pamoja na kanuni mbali mbali za mashindano, tukaishia kuzuiliwa kuvaa hata jezi zetu tulizo Kwenda nazo na kwa huruma tukasaidiwa na TFF kupata jezi zinazocomply na mashindano bado tukiporudi home tukaanza ugomvi wa kijinga wa haki ya kurusha mechi zetu wakati mambo yote yaliamliwa na kupitishwa na kikao cha Shirikisho la mpira Afrika ambacho hatukushiriki kwa uzembe wetu wenyewe.

-Leo tena dirisha la Usajili limefungwa, Yanga hawajawasilisha usajili wao TFF, usajili unaofanywa kupitia mfumo wa kisasa kupitia online application system maarufu kama 'TMS' (Transfer Merging System) , kwa mujibu wa TFF Yanga walipo alikwa Kwenye seminar ya Mafunzo ya namna Transfer Merging System inavyofanya kazi hawakupeleka muwakilishi, yaani mpaka Toto Afrika, Lipuli, Majimaji waliona umuhimu wa Mafunzo hayo Yanga hawakuona umuhimu wa kushiriki, nimesikiliza utetezi toka kwa kaimu katibu mkuu wa Yanga Baraka Desderbit amesema wao hawakushiriki kwasababu yeye hakuwepo na Jerry Muro alikuwa amefungiwa kwahiyo walikosa mtu wa kumpeleka kule Kwenye Mafunzo... hili ndio sababu ya Yanga kushindwa kushiriki Mafunzo haya muhimu kwa timu:kwakweli nimesikitika Sana kusikia utetezi huu Moja ya utetezi dhaifu na wa kijinga kabisa kuwahi kutolewa na Katibu Mkuu wa timu kama Yanga.

*MY TAKE *
-Toka Dr Tiboroa anafukuzwa na Manji timu imepwaya Sana Kwenye eneo la utendaji (Ofisi ya katibu mkuu) inashindwa kufanya kazi zake kikamilifu hata zile ndogo za kawaida ambazo hata timu za Lipuli FC toka Iringa zinatuzidi.

-Kaimu katibu mkuu wa Yanga Baraka Desderbit, Muhasibu huyu kitaluma toka Quality group, kijana mwenzetu hana uwezo wa kuwa katibu mkuu wa Yanga matukio haya yanayotokea Sasa ni ushahidi tosha kuwa boss wetu wa Secretarieti hatoshi, ni kweli wenda alikuwa Muhasibu mzuri pale Quality Group lakini Kuna utofauti mkubwa Kati ya kuendesha timu na kuwa Muhasibu wa kampuni binafsi.

-Washabiki wa Yanga tupunguze kumpigia makofi Manji kwa kila kitu anachosema tumfundishe kumkatalia na kusema hili sawa Lakin hili hapana bila hivyo atatupeleka shimoni.

-Mwisho boss wetu mkubwa tuliye mkodisha timu anapaswa kujua Yanga ni timu yenye umasikini mkubwa wa fedha lakini yenye utajili mkubwa Sana wa Mashabiki na wapenzi.. Kwa hiyo pesa sio kila kitu Kwenye timu, timu pia zinahitaji uongozi bora na Manji sio kiongozi bora wa timu bali ni mfadhiri bora hivyo anapaswa kupata katibu bora kama Dr Tiboroa,

Daniel Naftal Ngogo
Shabiki na mwanachama wa Yanga
Wakicheza na Manji watavuna mabua,maana kama Timu ikashushwa daraja ikaenda daraja la tatu ataendelea kuikodi?mambo ya menejimenti awaachie wanaojua,sasa anasema anaikodisha timu na ataigaia 25% hasara zote Yanga hawatausika,nimeshindwa kujua wanatumia Company law ipi?mbona Mo yeye kasema ananunua Hisa 51% kwahiyo Dunia nzima wanaelewa nini kitafuata,sasa Manji kakurupuka anasema anakodi sijui anatumia company law ipi sijui?
 
Kama wewe ni Mwanayanga kweli, nakupongeza kwa kuthubutu kutoa maoni mbadala bila ya kujali Wanayanga wengine watakuchukuliaje. Hata hivyo, kuna mambo ya msingi ambayo Mwanayanga wa kweli hawezi kuyasahau na kutozingatia kwenye swala hili, ila wewe umeyasahau na hukuyazingatia -labda kwa sababu ya Uyanga wako uliotukuka. Miongoni mwa hayo ni: (1) Kwenda mafunzoni Ghana siyo sababu pekee iliyomfukuzisha Tibohora. Kulikuwa na sakata la kuficha utetezi wa Niyonzima uliokaribia kumfukizisha timu. (2) Licha ya sifa za weledi alizo nazo Tibohora, ameonyesha udhaifu mkubwa wa kujiingiza kwenye kundi la Stand United lililopigwa na chini na TFF. Hii inaonesha kwamba binafsi Hana uwezo mkubwa kiasi anachodhaniwa, alibebwa na Taasisi ya Yanga aliyokuwa akiifanyia kazi. (3) TFF katika kipindi cha hivi karibuni imevaa sare ya misuguano na Yanga, chanzo kikuu kikiwa ni 'Diware' siku ya mechi na TP Mazembe na pesa za mgao kutolewa kwa hundi baada ya mechi na Modeama. Kwenye yote mawili TFF ndiye alikaa 'wrong site'. Kwa hivyo Mwanayanga yeyote angechukulia kauli yoyote ya TFF dhidi ya Yanga kwa tahadhari. (4) Transfer Matching system ni utaratibu endelevu (sustainable) unaohusisha taarifa za wachezaji wa timu zinazoshiriki mashindano yanayotambuliwa na FIFA. Kwa wachezaji wanaoendelea n timu zao, usajili wa msimu uliotangulia unaendelea. Kitachoshindikana ni wachezaji wanaohamia kutoka timu nyengine. Kusema kwamba wachezaji wa aina hiyo hawataruhusiwa kishiriki mashindano ya msimu mpya ni sahihi, kusema kwamba timu yote iliyocheza mashindano hayo msimu unaomalizika itafutwa ni TFF kulisha maneno mdomoni mwa FIFA. (6) n.k.
My take🙁1) Mtoa mada anaweza kuwa Yanga, lakini aliyekerwa na jambo kiasi kwamba anaitakia mabaya kwa kisingizio cha kauli ya TFF, la sivyo basi anaweza kuwa ni mnyama aliyejivika joho la kijani na manjanao. (2) TFF inatengeneza 'false dilemma' kwa Yanga ili kuikomoa na hatimaye kujifanya imetatua hiyo dilemma. (3) Lakini TFF hiyohiyo iko tayari kutumia kasoro yoyote ndogo itayofanywa na Yanga ili kuikomoa kwa kutumia mgongo wa FIFA. Kumbuka iliwahi kutaka kutumia mgongo wa TRA kutaka Yanga ilipishwe faini ya kuingiza watu bure mechi na TP Mazembe. Kumbuka imedaiwa kuwa TFF hiyohiyo iliwashawishi CAF kuiadhibu Yanga siku ya mechi hiyo kwa kuwa (eti) kulifanyika vurugu nje ya uwanja na kabla ya mechi. Visa hivi vya ukewenza dhidi ya Yanga havitaisha mpaka siku Yanga itapokubali kuburuzwa na TFF kuhusiana na maswala ya 'mkwanja'!
 
Wakicheza na Manji watavuna mabua,maana kama Timu ikashushwa daraja ikaenda daraja la tatu ataendelea kuikodi?mambo ya menejimenti awaachie wanaojua,sasa anasema anaikodisha timu na ataigaia 25% hasara zote Yanga hawatausika,nimeshindwa kujua wanatumia Company law ipi?mbona Mo yeye kasema ananunua Hisa 51% kwahiyo Dunia nzima wanaelewa nini kitafuata,sasa Manji kakurupuka anasema anakodi sijui anatumia company law ipi sijui?
Tuwe wakweli. (1) Hisa hununuliwa kwa kutegemea uwekezaji unaotaka kufanywa au kwanza kwa thamani ya kiliopo? (2) Asilimia ya umiliki wa hisa huamuliwa kwa idadi ya fedha inayowekezwa au kwa fedha iliyokwishawekezwa pamoja na mtaji? (3) Mali ya pamoja inapobadilishwa utaratibu wa kuiendesha ili kufuata mfumo wa hisa, wenye mali yao kwa pamoja huwa wanamiliki asilimia ngapi kama si mia moja kamili? Ni sahihi mmoja wa wamiliki hao kuamua apewe asilimia zaidi ya nusu kwa sababu tu atatoa fungu la kuimarisha mali hiyo? (4) Ni vipi itapatikana hiyo asilimia 51 ya kumpisha huyo aliyejitokeza kati ya wamiliki wanaoshiriki katika kumiliki asilimia 100 ya mali iliyopo? (5) Tunaelewa kwamba kumiliki asilimia 51 ya hisa ni kumiliki kura ya maamuzi dhidi ya 49 zilizobaki? Tunaelewa kwamba huko ni sawa na kuinunua kabisa mali yenyewe? Tunaelewa kwamba ikishakuwa hivyo hakutakuwa tena na kurudi nyuma? Tunaelewa kwamba wataopisha hiyo 51% ya hisa ili ziende kwa mwekezaji watakuwa wamejibadilisha maisha kutoka kuwa wanachama wenye haki ya maamuzi kuwa washabiki maandazi tu?....n.k.
Bila ya jawabu ya maswala hayo na kama hayo, kuwacheka wengine inaweza kuwa ni sawa na nyani kutoona .....le!
 
Nikianza na namba moja na mbili,(1&2)wewe unaijua Value ya Simba au ulishawahi kusikia washawai kufanya valuation ya Club yao?Mo kaja na thamani ni 20Billion katika 51% Simba nao waje na thamani yao ndio ulalamike
3.Kwani Simba ni mali ya nani?mbona Tanzania kwenye migodi haimiliki Hisa zaidi ya 51% wakati wana ardhi na wana madini.
4.Yeye kama mdau na mwanachama wa Simba kaomba lizaa kuiendesha Simba kwa kununua Hisa 51% kwahiyo kama kuna mwingine anaruhusiwa kuomba kwa kamati tendaji ya Simba ni tofauti na Yanga mwenyekiti kakaa kaamua Jumamosi anaikodi Yanga na Jumanne anataka asahinishwe wewe hapo unaona sawa kabisa!!kwanini asingeweka wazo lake mezani kama Mo aliwapa wazo mezani zaidi ya miezi mitatu kisha kasubili mkutano mkuu kashusha mzigo.
5.Bora ainunue tu ili tujue Simba ni mali ya nani kulikoni sasa pesa ya Okwi imeingia kwenye Account ya Simba kisha mtu mmoja anahamua kuihamishia kwenye account yake,hata kama alikuwa ana nia njema ya kuidhibiti,je baada ya kuihamisha angekufa unadhani familia yake wangetuelewa kama kuna pesa ya Simba kwenye account yake.Tubadilike ili tuende mbele
 
Kama wanachama wa yanga wangechangia 2000 TZS kwa mwezi mara * 8 mil tusingefika huku,tatizo watu wanapenda kwenda uwanjani na kuona timu inashinda kutoa ada ya uanachama hawataki unategemea timu itaendeshwa na mapato ya mlangoni? TFF na makato yake taifa yote mnayajua kinachobakia ni kidogo sana ndio timu zinapewa. Kama wanachama wangetoa 2000* 8mil =16 BL kwa mwezi huoni huo ni utajiri tulioukalia mpaka wafadhili wanatucheka?
 
nani kakudanganya yanga ina wanachama milioni 8?
 
Kama wanachama wa yanga wangechangia 2000 TZS kwa mwezi mara * 8 mil tusingefika huku,tatizo watu wanapenda kwenda uwanjani na kuona timu inashinda kutoa ada ya uanachama hawataki unategemea timu itaendeshwa na mapato ya mlangoni? TFF na makato yake taifa yote mnayajua kinachobakia ni kidogo sana ndio timu zinapewa. Kama wanachama wangetoa 2000* 8mil =16 BL kwa mwezi huoni huo ni utajiri tulioukalia mpaka wafadhili wanatucheka?
Yanga ina wanachama waliosajiliwa elf 12 na kati yao ni nusu au robo ndio wanalipia fees ambayo ni 1000 kwa mwezi, unaotaja wewe ni mashabiki wa yanga ambao kuwachangisha ni ngumu sana. Kutegemea chanzo hicho kuendesha timu basi umeipoteza rasmi kabisa kwani haitaweza kujiendesha hata kwa mwezi mmoja.
Yanga inahitaji muwekezaji mkubwa na mwenye nia ya dhati kuipeleka hatua nyingine kabisa.
 
Kama ni mashabiki tuchukue kadi sisi ni mtaji no 1
 
Hilo linawezekana kabisa ila kulifanya kuwa chanzo cha kuaminika ni kosa kubwa sana na kutaifilisi timu, watu wanaweza kuongea tu lakini waulize kwanin hawapeleki michango yao pale klabuni au ile juzi Manji alisema timu inahitaji kiasi cha Mil 500 kwa mwezi huu august ili kukamilisha uasjili, mishahara na maandalizi ya mechi 2 za kimataifa kwahiyo wale wanaozungumza kwenyw vyombo vya habar kuwa wanaweza kutoa hela nyingi basi waje hapa watoe hiyo hela. Kama kweli watu waliokuwepo pale walikuwa na huo moyo wangeanzia pale kudondosha hela hata mil 10 tu
 
Umesema kweli mkuu
 
Juventus ilishushwa na ikachukua ubingwa mara ngapi?...tena mfululizo
 
Back
Top Bottom