Mansa Musa: Mtu Tajiri zaidi duniani haijawahi tokea

zagarinojo

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2020
Posts
2,622
Reaction score
2,846
Je, wangapi wanafahamu historia ya Mansa Mussa mtu anayetajwa katika vitabu vya historia kuwa mtu tajiri zaidi duniani kuwahi kutokea.

Historia inasema alikuwa ni mfalme maarufu zaidi na aliyependwa katika ufalme wa Mali. Alirithi ufalme kutoka kwa mfalme Sundiata Keita, muanzilishi wa Mali empire ambayo zamani ilijulikana kama Kangaba.

Safari yake (Mansa Mussa) ya kwenda kuhiji huko Mecca ilkuwa yenye baraka na kustajabisha kwani Alibeba dhahabu nyingi na alikuwa akizigawa kwa watu alipokuwa njiani kipande kimoja tu cha dhahabu kilitosha kabisa kumtajirisha maskini.

Kwa wakati ule usingeweza kumlinganisha na Bill Gates, Dangote ama Jeff Besoz wa sasa.

Hakika ni historia kubwa.
 
Uzi haujautendea haki,

Naiman Davinci atapita hapa aifanye hii kazi vizuri ya kumuelezea mzee baba musa
 
Matajiri wapanda farasi hao🤣🤣🤣
Kila mtu tajiri kwenye Zama zake.
Tanzania-Mo,
Africa-Dangote,
India-Amban
Ulimwenguni--Jeff bezoes
Ndo tajiri ambaye mbaka vikaragosi vya mbinguni vinamjua.
 
Je, wangapi wanafahamu historia ya Mansa Mussa mtu anayetajwa katika vitabu vya historia kuwa mtu tajiri zaidi duniani kuwahi kutokea.

Historia inasema alikuwa ni mfalme maarufu zaidi na aliyependwa katika ufalme wa Mali. Alirithi ufalme kutoka kwa mfalme Sundiata Keita, muanzilishi wa Mali empire ambayo zamani ilijulikana kama Kangaba.

Safari yake (Mansa Mussa) ya kwenda kuhiji huko Mecca ilkuwa yenye baraka na kustajabisha kwani Alibeba dhahabu nyingi na alikuwa akizigawa kwa watu alipokuwa njiani kipande kimoja tu cha dhahabu kilitosha kabisa kumtajirisha maskini.

Kwa wakati ule usingeweza kumlinganisha na Bill Gates, Dangote ama Jeff Besoz wa sasa.

Hakika ni historia kubwa.
Aluzipata wapi hizo mali alizokua anamiliki? Yaani rasilimali za nchi ninyi mnasema ni mali za mtu!
 
Aluzipata wapi hizo mali alizokua anamiliki? Yaani rasilimali za nchi ninyi mnasema ni mali za mtu!!
Huyu history inasema alikuwa mfalme, na alikusanya ushuru kwa sababu njia kuu ya wafanyabiashara ilipita kwenye himaya Yake. Sasa alivyokuwa bogus akachukua Mali nyingi na msafara mkubwa Sana akasafiri kwa anasa Sana kwenda kuhiji. Utawala wake ukafirisika ndo ukawa mwisho wake.
 
Unajua mfano Jeff Bezos tajiri wa sasa wa dunia, utajiri wake ni almost $200B lakini thamani ya amazon kwa sasa ni almost $1Trillion.

So hapo maana yake Jeff katengenezea utajiri watu wengine wenye thamani ya almost $800B.

Sasa huyo Mansa Musa kaboresha vipi maisha ya watu wake ambalo ndilo lilikuwa jukumu lake la kwanza.
 
Back
Top Bottom