Mantiki ya hii makala ya Balile ni aina ya mikopo iliyokopwa wakati wa Hayati Magufuli

Linguistic

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2021
Posts
3,669
Reaction score
8,268
Siku zote Miradi ya Maendeleo kwa kanuni za kiuchumi mara zote ama mara nyingi hutumia zaidi concessional loans na siyo commercial loans.

ROIs kwa miradi hii huwa inachukua muda mrefu ndiyo maana ushauri wa kitaalam huelekeza mikopo itoke ktk Benki za Maendeleo na siyo za Biashara.

Benki hizo hutoza riba ndogo sana na pia hutoa grace period ya takribani miaka 5 na muda wa marejesho huwa ni miaka mingi (20-50).

Ilihali benki za kibiashara hutoza riba kubwa, grace period ya mwaka na muda wa marejesho ni mfupi. Mikopo hii inafaa kwa ajili ya miradi ya uzalishaji zaidi kama vile ujenzi wa viwanda na mambo yenye kuweza kutengeneza hela za haraka haraka.

Reli, barabara, umeme, ujenzi wa majengo ya huduma za kijamii ni baadhi ya mambo/ miradi inayochukua muda mrefu kurejesha faida ya uwekezaji ambapo kama umechukua mkopo kutoka Benki hizi za kibiashara hutoweza kumudu madeni husika.

The other development financing options badala ya kukopa kutoka kwenye Benki za Kibiashara ni kupitia PPP (Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi).

Tuna Sera, Mkakati wa Utekelezaji wa Sera, Sheria, Kanuni na Miongozo tangu mwaka 2009 (binafsi nimeshiriki mchakato wa uandaaji wa hizi nyaraka) lakini hadi leo hii mradi pekee wa wazi uliokamilika na wenye kutumia huu mfumo wa PPP ni huu wa BRT (mwendokasi - Dar) japo wenyewe ni mkopo wa Benki ya Dunia lkn uendeshaji wake ni PPP.

So far mafanikio ya BRT yapo chini ya malengo na kwa mtazamo wangu ni kwamba Serikali iliingia bila kujiandaa maana mchakato wa manunuzi haukufuata misingi mahususi ya mfumo wa PPP.

Serikali ikiweka National Negotiation Team thabiti tungeweza kuokoa pesa nyingi kupitia PPPs.

Maana kinachotakiwa ni kuwa na terms nzuri za win-win situation ili mwenye mtaji (mwekezaji) apate na Serikali mwisho wa siku nayo ipate/ifaidike.

I stand to be corrected Guys [emoji120][emoji120][emoji3048][emoji120]

PIA, SOMA:
- Balile: Magufuli katutenda, deni la nje lafikia shilingi Trillion 78
 
Hapa ni kuweka mkazo familia yote ya magufuli isipate uongozi nchi hii, hawa watakuwa na roho kama za baba yao
Nchi ni ya kwako na baba yako au?

Utashangaa unafulahi utakapo ona wanakuja kuchumbia kwenu au wengine kuwa baba yako.

Hapo utakaa kimya bila kerere na kutikisa mkia.
 
Deni la trillion 77 siyo la miaka mitano bali ni cumulative na humohumo kubadwni la private sector la dolla 5billion. Someni BoT report muone madeni by march 2021 na by DEC 2015, halafu linganisha kila laini
 
Nilisha post humu kitambo sana, ni kwa nini sisi kama nchi tunafurahia sana kukopa na kulipa ni majanga? Ifikie wakati sisi kama nchi tuwe na mikakati na njia ya kuhakikisha tunakuwa self sufficeint kila kona. Hivi ndivyo walivyoanza nchi za Asia- kama Thailand, yaani kuwa self sufficeint kwanza kwenye chakula, barabara, huduma za afya.

Kulipa madeni yao yote ya nje na ilianzishwa kodi maalumu ya kulipia madeni, yaani kwa mfano kila mtu atalipa Tsh 100 kila mwezi kulipa mikopo, halafu tuwe na independent tax payers alliance ili kujua hiyo mikopo kama imetumika kama ilivyokusudia na kama malipo yanafanyika kama yavyotakiwa, sio hizi habari za tunakopesheka, halafu kulipa inakuwa kutafutana. Hii habari za Balile ni kama wamemtuma aje kupima upepo.
 
Uwawekee waTZ hawa 100 kila mwezi unajua kelele watazopiga huku wakisapotiwa na hao wanaojiita "wapinzani"? Hiki ulichoeleza kinatekelezeka kwenye nchi zenye raia na viongozi wanaojielewa...
 
Sasa kwa nini wanafurahia na waendelee kukopa wakati uwezo wa kuzirejesha hawana, si afadhali tu waombe grants bila marejesho...?
 
Siku zote Miradi ya Maendeleo kwa kanuni za kiuchumi mara zote ama mara nyingi hutumia zaidi concessional loans na siyo commercial loans.

ROIs kwa miradi hii huwa inachukua muda mrefu ndiyo maana ushauri wa kitaalam huelekeza mikopo itoke ktk Benki za Maendeleo na siyo za Biashara.

Benki hizo hutoza riba ndogo sana na pia hutoa grace period ya takribani miaka 5 na muda wa marejesho huwa ni miaka mingi (20-50).

Ilihali benki za kibiashara hutoza riba kubwa, grace period ya mwaka na muda wa marejesho ni mfupi. Mikopo hii inafaa kwa ajili ya miradi ya uzalishaji zaidi kama vile ujenzi wa viwanda na mambo yenye kuweza kutengeneza hela za haraka haraka.

Reli, barabara, umeme, ujenzi wa majengo ya huduma za kijamii ni baadhi ya mambo/ miradi inayochukua muda mrefu kurejesha faida ya uwekezaji ambapo kama umechukua mkopo kutoka Benki hizi za kibiashara hutoweza kumudu madeni husika.

The other development financing options badala ya kukopa kutoka kwenye Benki za Kibiashara ni kupitia PPP (Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi).

Tuna Sera, Mkakati wa Utekelezaji wa Sera, Sheria, Kanuni na Miongozo tangu mwaka 2009 (binafsi nimeshiriki mchakato wa uandaaji wa hizi nyaraka) lakini hadi leo hii mradi pekee wa wazi uliokamilika na wenye kutumia huu mfumo wa PPP ni huu wa BRT (mwendokasi - Dar) japo wenyewe ni mkopo wa Benki ya Dunia lkn uendeshaji wake ni PPP.

So far mafanikio ya BRT yapo chini ya malengo na kwa mtazamo wangu ni kwamba Serikali iliingia bila kujiandaa maana mchakato wa manunuzi haukufuata misingi mahususi ya mfumo wa PPP.

Serikali ikiweka National Negotiation Team thabiti tungeweza kuokoa pesa nyingi kupitia PPPs.

Maana kinachotakiwa ni kuwa na terms nzuri za win-win situation ili mwenye mtaji (mwekezaji) apate na Serikali mwisho wa siku nayo ipate/ifaidike.

I stand to be corrected Guys
emoji120.png
emoji120.png
emoji3048.png
emoji120.png

PIA, SOMA:
- Balile: Magufuli katutenda, deni la nje lafikia shilingi Trillion 78
Hiyo national negotiation team haitakula rushwa kama ilivyo desturi za wenye dhamana wengi kufanya ufisadi?

PPP haifai kabisa kutokana na ukweli haiwezekani hata kidogo wakati wa uingiaji mikataba hiyo maslahi ya nchi yakazingatiwa na hao wanaowakilisha upande wa serikali. Ĺabda PPP iwe kati ya taasisi ya umma kana vile mifuko ya hifadhi na serikali lakini sio na watu binafsi. Gharama halisi za miradi huwa inflated sana ili waibe na kwa baraka za timu ya upande wa serikali.
 
  • Thanks
Reactions: Ame

Taasisi ya umma na Serikali duh basi sawa mkuu. Taasisi ya umma ni Taasisi ya Serikali. Bad enough leo hii Serikali inadaiwa 4.6 trillion na mifuko ya pensheni. Tuliiokoa PSPF kisiasa kwa kuunganisha mifuko mingine 4 lakini technically tuliishabugi.

Rushwa haiwezekani kuisha siyo Tz tu bali dunia nzima LAKINI inawezekana ikapunguzwa iwapo tu kuna mifumo sahihi na imara na kwa Tz hili bado sana kwasababu tu maamuzi ni ya mtu mmoja asiyepingwa. Na hili litaendelea kuwa janga la kitaifa lisilotamkwa ama kudhibitiwa na Sheria za nchi.

Kwa ufupi, negotiation team siyo decision makers na makubaliano yao siyo binding pitia tools zilizopo zipo wazi tu mbona.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Grants zitatosha kujenga SGR? Bwawa la umeme?
Watachanganya na private investors- yaani PPP- public Private Partnerships, dunia hii ya nini kugangamara na mamiradi yanayotegema mikopo yenye masharti ya kuinamishwa kila corner?
 
Back
Top Bottom