Kelvin Wills
New Member
- Jun 14, 2024
- 1
- 2
Elimu ya sheria imekua ikiipuuzwa sana katika sekta ya elimu Tanzania ama imekua haipewi kipaumbele sana hivyo imepelekea kuwepo kwa matukio ambayo yanarudisha nyuma maendeleo ya taifa, maadili duni ya wananchi, viongozi wasio na sifa, pamoja na usalama wa nchi kuwa matatani kwa ujumla. Je mtanzania elimu ya sheria inakusaidiaje?
Elimu ya sheria ni ya msingi kwa sababu inasaidia kutambua haki na wajibu wako kama mtanzania. Matendo mengi ya uvunjifu wa sheria yanatokea kWA SABABU watu hawafahamu au wanapuuzia sheria za nchi na hivyo inapelekea upotevu wa amani, kukosekana kwa haki kwenye vyombo vya umma pamoja na uonevu kwa wanyonge.
Kauli "kutokujua sheria si kisingizio" inamaanisha kwamba mtu hawezi kudai kutokuwa na hatia kwa sababu hajui sheria. Hii ni kwa sababu inahimiza watu kujifunza na kufuata sheria, kuhakikisha usawa na haki, na kuimarisha utawala wa sheria. Hivyo basi endapo utaenda kinyume na sheria haijalishi kwamba elimu yako juu ya sheria itakuokoa ni muhimu kujifunza sheria.
Ili kujenga jamii bora ni muhimu sana kufahamu sheria, hii inasaidia kutambua mienendo ya viongozi wetu katika jamii zetu pamoja na njia za kufanya maamuzi ya busara yatakayo tusaidia kujenga taifa lenye muhimili bora. Yametokea matukio mbali mbali katika jamii ambayo kwa namna moja au nyingine yangeweza kuharibu mstahimili wa jamii kama vile rushwa, viongozi kutumia mamlaka vibaya na kuwakandamiza wanyonge pamoja na mambo mengine mengi yasiyo faa na bila shaka wanao umia ni tabaka la wanyonge wasiojua sheria.
Hivyo basi ni wajibu wa kila mtanzania kuja sheria japo kwa kiasi flani ili aweze kuenenda vizuri kwa ajili ya maendeleo binafsi na ya taifa kwa ujumla.
Hizo ni baadhi ya faida za kuijua sheria kama mtanzania. Yafuatayo ni makundi ya msingi ambayo kama mtanzania inabidi uyafahamu kwa ajili ya ustawi wa jamii.
i. Sheria za Jinai (Criminal Law): Zinahusu makosa na adhabu zinazotolewa kwa vitendo vya jinai kama vile wizi, unyanyasaji, mauaji, na uharibifu wa mali.
ii. Sheria za Kiraia (Civil Law): Zinashughulikia migogoro kati ya watu binafsi au taasisi, kama vile migogoro ya mikataba, migogoro ya ardhi, na madai ya fidia.
iii. Sheria za Familia (Family Law): Zinajumuisha masuala yanayohusiana na ndoa, talaka, utunzaji wa watoto, na urithi.
iv. Sheria za Ajira na Kazi (Employment and Labor Law): Zinahusu haki na wajibu wa waajiri na waajiriwa, kama vile mshahara wa chini, mazingira ya kazi, na ulinzi wa haki za wafanyakazi.
v. Sheria za Ardhi na Mali (Property Law): Zinashughulikia umiliki wa ardhi na mali nyingine, uhamishaji wa mali, na masuala ya upangaji.
vi. Sheria za Biashara (Commercial Law): Zinahusiana na uendeshaji wa biashara, mikataba ya kibiashara, na ushindani.
vii. Sheria za Haki za Binadamu (Human Rights Law): Zinajumuisha haki za kimsingi ambazo kila mtu anastahili, kama vile haki ya kuishi, uhuru wa kujieleza, na usawa mbele ya sheria.
Kwa ujumla, kuwa na ufahamu wa makundi haya ya sheria kunawawezesha raia kuishi kwa amani, kujilinda dhidi ya dhuluma, na kuchangia katika maendeleo ya jamii.
Je ni nini kifanyike ili kuhakikisha elimu juu ya sheria mbali mbali za nchi zinamfikia kila mtanzania?
Kwa kuwa tumepata kuona faida mbali mbali za kuifahamu sheria na kuishi kulingana na mwongozo wa sheria basi ni vyema serikali pamoja na mashirika mbali mbali yanayohusika na utoaji wa elimu kwa jamii kuhakikisha suala hili linatiliwa mkazo sana hivyo yafuatayo ni baadhi ya mambo ya kuzingatia ili kujenga Tanzanian bora kwenye nyanja hii;
i. Elimu juu ya sheria inapaswa ifundishe kuanzia ngazi za chini/msingi (primary level) mpaka vyuoni (secondary and college/university level) kama somo la lazima (compulsory) hii itasaidia vijana kuwa na uelewa juu ya sheria za nchi na kuziishi pia wataweza kutambua ni mwenedo upi unaofaa kwa mtanzania.
ii. Pia, kuwepo na uusishwaji wa jamii (Community engagement) kwenye kutunza sheria za nchi hasa hasa kwa kutengeneza kamati maalumu zitakaso simamia sheria ndogo ndogo kwa nyanja ya jamii ili kuleta mabadiliko na kuibua viongozi bora.
iii. Viongozi wa nchi pia wapitishwe kwenye sheria za nchi kwani huenda wengi wao wanatenda mambo bila kutambua sheria inasemaje.
Mwisho ni haki yako ya msingi kujua sheria za nchi yako kama mtanzania ili kuisaidia kupata maendeleo siku zijazo.
Asanteni sana kwa kusoma ujumbe huu.
Imeandaliwa na KELVIN WILSON.
#stories of change 2024.
#Tanzania tuitakayo.

Upvote
4